Watu 16 wafariki kwenye ajali ya ndege Marekani
Watu 16 wafariki kwenye ajali ya ndege Marekani
Takriban watu 16 wamefariki kwenye ajali ya ndege ya jeshi kwenye jimbo la Mississipi nchini Marekani.
Watu wote 16 waliokuwa ndani ya ndege hiyo waliangamia.
Hakuna taarifa rasmi zilizotolewa kuhusu kilichosababisha kutokea ajali hiyo.
Kwa mujibu wa jarida la jimbo la Mississipi ni kuwa ndege hiyo ilianguka katika shamba moja na mabaki yake yakatabakaa mbali.
No comments