Header Ads

ad

Breaking News

Chanjo ya ugonjwa wa kisonono yapatikana

                  Gonorrhoea imekuwa taabu kutibika kwa sababu imezoea antibiotic 
 
Wanasayansi nchini New Zealand wameonyesha kwa mara ya kwanza kwamba chanjo inaweza kutoa kinga dhidi ya ugonjwa wa kisonono.


Watafiti kutoka chuo kikuu cha Auckland wamegundua kuwa maambukizi ya ugonjwa huo wa zinaa yameshuka kwa takriban theluthi moja miongoni mwa watu ambao walipata chanjo dhidi ya homa ya manjano.

Watafiti hao wamefuatilia kutoka kwa vijana milioni moja waliopata chanjo hiyo pindi kulipotokea ugonjwa wa homa ya manjano nchini New Zealand.
 
Tiba ya sasa ilikuwa inadumu kwa miaka miwili pekee
Kisonono imekuwa taabu kutibika kwa sababu imezoea dawa za antibiotic.
Mwandishi wa BBC wa masuala ya afya anasema utafiti huu unaonyesha inawezekana kuwa na chanjo dhidi ya ugonjwa.

No comments