Header Ads

ad

Breaking News

KOCHA MAYANGA ATANGAZA KIKOSI CHA TIMU YA TAIFA KITAKACHOIVAA RWANDA, AWAONGEZA SITA WAPYA

Kocha wa Stars, Salum Mayanga

                                                           Mwandishi Wetu

KOCHA Mkuu wa timu ya Taifa (Taifa Stars),Salum Mayanga amewaongeza wachezaji sita katika kikosi kitakachoivaa Rwanda Alhamisi kwenye Uwanja wa CCm Kirumba mkoani Mwanza.

Katika kikosi hicho amewaacha kipa wa Yanga, Benno Kakolanya, Mbaraka Yusuph na Shaban Idd kutokana na sababu mbalimbali, huku Himid Mao akizubiri hatma yake ya kucheza soka nje ya nchi.


Mayanga amewataja wachezaji wapya ni kipa Serengeti Boys, Ramadhani Kabwili, Joseph Mahundi, Kelvin Sabato, Athanas Mdamu, Said Ndemla na Boniface Maganga.
wapya hao wanaungana na wengine walioshiriki Michuano ya Cosafa, kwa ajili ya kusaka tiketi ya kucheza fainali za Afrika kwa Wachezaji wa Ligi za Ndani (Chan), zitakazofanyika mwaka 2009 nchini Ivory Coast.

Kikosi kilichoondoka leo kipa Aish Manula,Said Mohammed na Kabwili, wakati mabeki ni Shomari Kapombe, Hassan Kessy, Gadiel Michael, Hamimu Abdul, Maganga, Salim Mbonde, Abdi Banda na Nurdin Chona.

Mayanga amewatangaza viungo ni Mzamiri Yassin, Mao, Salmin Hoza, Raphael Daud, Erasto Nyoni, said Ndemla, Simon Msuva, Shiza Kichuya na Mahundi, huku wapachika mabao wakiwa ni Athanas Mdamu, John Bocco, Kelvin Sabato na Stamil Mbonde.



No comments