GS WARRIORS BINGWA MPYA NBA, WAITANDIKA CLEVELAND 129-120
KEVIN DURANT alikuwa katika kilele
 cha umahiri wake kwa kuisaidia timu yake ya Golden State Warriors 
kutwaa ubingwa wa Ligi ya Basketball ya Marekani (NBA) dhidi ya mahasimu
 wao Cleveland Cavaliers katika mchezo uliomalizika alfajiri ya leo kwa 
saa za Afrika Mashariki.
Mchezaji huyo alifunga pointi 39 katika mchezo wa vuta-nikuvute uliomalizika kwa ushindi kwa pointi 129 kwa 120.
Stephen Curry aliongeza point 34, 
pasi za mwisho 10 na mipira sita aliyoitumbukiza kwenye neti baada ya 
kugonga ubao.  Warriors walijihakikishia ushindi huo kufuatia kushinda 
mchezo wa saba wa mfululizo wa 4 kwa 1, hivyo kunyakua tena ubingwa wake
 wa pili katika miaka mitatu baada ya kushindwa kwa 3 kwa 1 mwaka 
uliopita.    
 
 







 
 
 
 
 
 
 
 
 
No comments