Tanzania yabeba medali 11 michuano ya SARPCCO Swaziland
Wanariadha wa Tanzania walioshiriki michezo ya majeshi ya
Polisi kwa nchi za Kusini mwa Afrika(SARPCCO) katika mji wa Mbabane
nchini Swaziland wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kumaliza michezo
hiyo.(Picha na Frank Geofray wa Jeshi la Polisi-Swaziland)
Wanariadha wa mbio za nyika (KM 10) kutoka Polisi Tanzania
wakifurahia baada ya kuvalishwa medali ya ushindi wa jumla katika mbio
hizo wakati sherehe za kufunga michezo ya majeshi ya Polisi kwa nchi za
Kusini mwa Afrika(SARPCCO) katika mji wa Mbabane Swaziland.(Picha na
Frank Geofray wa Jeshi la Polisi-Swaziland)
………………………………………………………………………………..
………………………………………………………………………………..
Na. Frank Geofray-Jeshi la Polisi,Swaziland.
Timu ya
wanariadha wa Polisi Tanzania waliokuwa wakishiriki michezo ya majeshi
ya Polisi kwa nchi za Kusini (SARPCCO) nchini Swaziland imefanikiwa
kumaliza michezo hiyo, huku ikipata jumla ya medali kumi na moja na
hivyo kufanikiwa kushika nafasi ya tatu katika mchezo wa riadha.
Timu hiyo
imefanikiwa kupata medali sita za dhahabu, tatue za fedha na mbili za
shaba kutokana na wanariadha wake kumi na mbili walioshiriki michezo
hiyo iliyoshirikisha jumla ya nchi kumi na tatu huku nafasi ya kwanza
ikichukuliwa na Zimbabwe ikifuatiwa na Namibia.
Michezo hiyo
ilifungwa jana na Waziri wa Katiba na sheria wa Nchi ya Swaziland
Mhe.Seneta Hillary ambapo katika hotuba yake alisisitiza umoja na
ushirikiano kupitia michezo kwa nchi wanachama wa umoja huo pamoja na
kuzipongeza nchi zote zilizoshiriki na kuleta ushindani mkubwa.
Hillary
alisema michezo hiyo imekuwa fursa kubwa ya kuwakutanisha wanamichezo wa
majeshi ya Polisi hivyo amewaomba wakuu wa majeshi ya Polisi na nchi
wanachama kuyapa umuhimu na kipaumbele michezo hiyo ili kuwawezesha
askari polisi kubadilishana mbinu za kukabiliana na uhalifu pamoja na
kujenga afya zao.
Akizungumzia
matokeo hayo, Mkuu wa Kitengo cha Michezo wa Jeshi la Polisi, Mrakibu
Mwandamizi wa Polisi SSP Jonas Mahanga amesema michezo hiyo ilikuwa na
ushindani mkubwa lakini timu ya Tanzania ilijitahidi na kujituma hivyo
kufanikiwa kufanya vizuri ukilinganisha na timu nyingine zilizoshiriki
micvhezo hiyo.
“Nawapongeza
wachezaji wetu wa Tanzania wote kwa kazi nzuri waliyofanya hivyo
kurejea na ushindi wa medali kumi na moja nyumbani na katika michezo
mingine tunaendelea kujipanga vyema ili kufanya vizuri zaidi”Alisema
Mahanga.
Timu hiyo inatarajia kurejea Tanzania siku ya Jumanne jioni kwa ndege ya shirika la Afrika kusini.
No comments