Lowassa atikisa mkoani Mbeya
 Mgombea urais
 kupitia vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya wanchi (UKAWA), Edward 
Lowassa,akaiangalia bila kuamini idadi kubwa ya wananchi waliojitokeza 
kumsikiliza baada ya kufanya ziara ya kusaka wadhamini kwa mikoa ya 
Nyanda za juu kusini, hapo ilikuwa kabla ya kuwahutubia wananchi 
waliojitokeza kwa wingi katika viwanja vya Luanda Nzovwe, Jijini Mbeya 
Jana.
 ......................................................................................................................................................
Mgombea urais kupitia vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya wanchi (Ukawa), Edward Lowassa,
amasema endapo atachaguliwa kuwa Rais hatakuwa na mchezo na watu wasiopenda
maendeleo na kwamba ameahidi kubadili utaratibu wa utendaji kazi nchini ka watu
kufanya kazi kwa saa 24, tofauti na ilivyosasa kwani hali hiyo inafanya uchumi wan
chi kutochangamka.
Aliyasema hayo
jana Jijini hapa alipofanya ziara ya kutafuta wadhamini kwa mikoa ya nyanda za
juu kusini, ambapo baada ya kukabidhiwa orodha ya wadhamini alihutubia maelufu
ya wakazi wa Mbeya, katika viwanja vya Luanda Nzovwe.
Lowassa aliyeanndamana
na mkewe na mgombea Mwenza Juma Dun Haji, pamoja na viongozi mbalimbali wa
UKAWA , pia alisema kazi nyingine atakayoifanya baada ya kuingia madarakani ni
kuugeuza mkoa wa Mbeya kuwa mji wa Kimataifa na bakuwa kitovu cha uchumi
unaosisimka kama ilivyo baadhi ya miji maarufu ya Ulaya.
“Nataka
niwaambie niataubadilisha mji wa Mbeya kuwa wa kimataifa , kuwa kama  Nairobi na Uswis kwa kutumia zaidi uwanja wa
kimataifa wa Songwe, Mbeya mji wenye uchumi wa kisasa” alisema Lowassa.
Mbali na
ahadi hiyo kwa Mkoa wa Mbeya, Lowassa aliendelea kuwapaa matumani wananchi kwa
kusema kuwa, akifanikiwa kushika dola ataunda serikali rafiki na wananchi wa
kipato cha chini kama wamachinga, Bodaboda na Mama ntilie.
Lowasa pia
alisema akiwa madarakni atamwachia mwanamziki maarufu aliyefungwa jela maisha
kwa kosa la ubakaji, pamoja na familia yake< nguza Vicking (Babu Seya).
Alilazimika kutoa
ahadi hiyo baada ya wananchi kuhoji juu ya mwanamziki huyo, ambapo wakati
Lowassa akiaga baada ya kueleza mambo atakayoshughulika nayo, ghafla wananchi
walipiga mayowe wakihoji babu Seya je, ndipo Lowassa aliamua kuahidi kuwaachia
huru.
Awali awali
akimkaribisha mgombea huyo, Menyekiti mwenza wa Ukawa, Freeman Mbowe, alitumia
fursa hiyo kuonya juu ya mambo mawili kuelekea katika uchaguzi wa Oktoba 25
mwaka huu.
Mbowe
alisema suala la uchakachuaji wa majina ya vijana katika daftari la wapiga kura
ni hatari na kuomba Tume ya Taifa (NEC) kuepuka kufanya jambo hilo kwani
litasababisha vurugu kubwa  kwa kuwa
tayari kuna viashiria hivyo.
Pia alilitaka
jeshi la polisi kuepuka na kuendeleza tabia ya kuwa wakala wa Chama cha
Mapinduzi (CCM) na badala yake kukaa upande wa pili wa historia kwa kuwa
wananchi wanahitaji mabadiliko.
Makada wapya toka CCM
Mbowe
alitumia mkutano huo kuwatambulisha makada wapya waliojiunga na chama hicho
kutoka CCM ambao ni mbunge, Modestus Kiluf wa Mbarali, Mchungaji Luckson
Mwanjale ambaye hata hivyo hakupanda jukwaani kukabidhiwa kadi, pamoja na
Mwanasiasa mkongwe, Njelu Kasaka.
Kwa upande
wake, Mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi ambaye alikuwa mwenyeji , aliwatuhumu
viongozi wa CCM kuwa wameingiza shahada bandia za kupiga kura kwa lengo la
kuchakachua kura Oktoba 25 Mwaka huu.
Alisema kuwa, kwa mujibu wa taarifa zilizoifikia
Chadema ni kwamba kura shahada hizo za bandia ziliingizwa Mkoani Mbeya kutoka
Mkoani Dodoma na  kwamba tayari  chama hicho kimeandaa mkakati wa
kuhakikisha shahada hizo hazitumiki ili kuisaidia CCM kushindi.
Mbatia
Mwenyekiti
wa NCCR-Mageuzi, James Mbatia, akihutubia katika mkutano huo alisema 
licha ya Rais Jakaya Kikwete kusema kuwa ni maadui wao wataendelea kuhubiri
amani ili kujenga matumaini kwa wananchi ambao tayari wanahitaji mabadikiko.
"Tarehe 4 mwezi huu Rais Kikwete alituita
wapinzani ni maadui, sisi tutaendelea kuhubiri amani, kuhubiri uungwana na watu
wa Mbeya mmeweka historia na naomba wanambeya tusijaribu kuhubiri chuki "
alisema Mbatia.
Alisema kuwa taifa linaviashiria vyote vya
kugawanyika  ndio maana UKAWA wameamua kumsimamisha Lowassa  kugombea
nafasi ya Urais jwa kuwa ndiye mtu pekee kwa sasa ndio anaweza kulirudisha
taifa katika misingi yake ya umoja na amani.
Hali ilivyokuwa kabla
na baada ya lowassa kuwasili Mbeya
Lowassa aliyewasili katika uwanja wa ndege majira ya
saa 8:30 za mchana alilazimika kutumia muda wa saa mbili na nusu kutoka
uwanjani wa ndege wa Songwe hadi eneo lililoandaliwa kwa ajili ya mkutano la
Ruada Nzovwe umbali wa kilomita 30.
Hali hiyo ilisababisha askari polisi kufanya kazi ya
ziada kumnasua kiongozi huyo kutoka katika makundi ya watu waliosimama
barabarani kuzuia msafa wake kutoka uwanja hapo.
Ndani ya uwanja wa ndege wakati Lowassa anasubiriwa
walijitokeza makada wa Chama cha Mapinduzi(CCM) ambao pia walikuwa wagombea
ubunge na wabunge waliomaliza muda wao, Mchungaji Luckson Mwanjale aliyekuwa
mkombea ubunge jimno la Mbeya vijijini na Dickson Kilufi wa Mbarali.
 


 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
No comments