BONNY MWAITEJE AITIKISA DIAMOND JUBILEE

Mwimbaji nguli wa muziki wa
injili Bonny Mwaitege akiimba
katika uzinduzi wa albam zake kwenye
ukumbi wa Diamond
Jubilee jijini Dar es Salaam jana, uzinduzi ambao
ulihudhuriwa na
maelefu ya wapenzi wa muziki wa ijini akishirikiana na
waimbaji mbalimbali wa
muziki huo ikiwa ni pamoja na baadhi ya kwaya
kutoka katika baadhi ya
makanisa ya jijini Dar es salaam, Bonny Mwaiteje
alikonga nyoyo za mashabiki
wake kwa ikwango kikubwa huku akiwa
amevalia vazi la Kinigeria wakati akiwa
jukwaani, wapenzi wa ,muziki
waliohudhuria katika uzinduzi huo walijikuta kila
mmoja akijitikisa pale
alipo kutokana na kuvutiwa na nyimbo za mwimbaji huyo
kutoka mkoani mbeya.(PICHA NA KIKOSIKAZI CHA FULLSHANGWE-DAR ES SALAAM)

Mwimbaji nguli wa muziki wa
injili Bonny Mwaitege akitunzwa na wapenzi
mbalimbali wa muziki wa
injili wakati alipokuwaa akiimba jukwaani.

Baadhi ya maaskofu na wachungaji waliohudhuria katika uzinduzi huo
wakifuatilia wakati mwimbaji huyo akiimba jukwaani.

Mwimbaji nguli wa muziki wa injili Bonny Mwaitege akifanya mabo
makubwa jukwaani.

Baadhi ya wapenzi wa muziki wa injili wakiwa katika uzinduzi huo.

Askofu na Dokta Mwakibolwa wa
EAGT pamoja na maaskofu
wengine wakiombea albam hizo kabla ya
kuzizindua rasmi kushoto ni
Alex Msama
Mkurugenzi wa Kamuni ya Msama
Promotion.

Baadhi ya wafanyakazi wa Kampuni ya Msama Promotion wakishiriki
katika sala.

Sala ikiendelea kabla ya kuzinduz albam hizo.

Baadhi ya wapenzi wa muziki wa injili wakiwa katika uzinduzi
huo uliofanyika
jana kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee.

Askofu na Dokta Mwakibolwa wa EAGT akizindua rasmi albam hizo kushoto
Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotion Bw. Alex Msama.

Maaskofu na wachungaji wakiwa wameshikilia albam zao mara baada ya
kukabidhiwa na Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotion.


Wafanyakazi wa Msama Promotion wakiwa katika picha ya pamoja.
No comments