Bondia Lulu aibuka mshindi Afrika Kusini
Rais wa TPBO, Yassin Abdallah 'Ustadhi' akimnyoosha mkono juu bondia Lulu Kayage baada ya kuibuka mshindi katika pambano lake dhidi ya bondia wa Afrika Kusini.
BONDIA wa Kike Lulu Kayage mwishoni mwa wiki iliyopita alibuka kidedea nchini Afrika ya kusini baada ya kumdunda Lizbeth Sivhaga wa nchini humo.
Hilo ni pambano lake la kwanza kucheza nje ya nchi na kufanikiwa kushinda kwa T.K.O ya raundi ya pili, mchezo ulioanza kwa mashambulizi huku kila mmoja akitaka kumpiga mwenzake katika raundi za awali.
Hata hivyo, ilivyofika raundi ya pili bondia Lulu alimwelemea mpinzani wake kwa makonde mfululizo na wasaidizi wake wakamwokoa kwa kumtupia taulo hivyo, kumpa Lulu ushindi T.K.O ya raundi ya pili.
Ushindi wa Lulu ulichagizwa na kocha maarufu nchini, Rajabu Mhamila 'Super D', ambapo siku mbili kabla ya kuondoka nchini, alimzawadia vifaa mbalimbali vya mchezo wa masumbwi na kumwahidi ushindi kwa asilimia zote.
bondia huyo anatarajia kurudi nchini leo kwa ajili ya maandalizi ya mapambano yake mengine ya kimataifa, lakini bondia Ramadhani Shauri alipoteza pambano lake kwa kupigwa K.O ya raundi ya nne na bondia Philip Ndlovu wa Afrika ya Kusini. Pambano hilo lilikuwa la raundi nane.
No comments