Header Ads

ad

Breaking News

Azam FC mabingwa Kagame, yailiza Gor Mahia 2-0

Mgeni rasmi katika fainali za Kombe la Kagame kati ya Azam FC na Gor Mahia, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Saidi Sadiki (wa tatu kulia), akiwa pamoja na viongozi wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika Mashariki na Kati (CECAFA), wakati nyimbo za Taifa za Tanzania na Kenya zikiimbwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam leo. (Picha zote na Kassim Mbarouk-www.bayana.blogspot.com)
Mgeni rasmi katika mchezo wa fainali za Kombe la Kagame kati ya Azam FC na Gor Mahia, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Saidi Sadiki, akisalimiana na kukagua timu ya Azam FC kabla ya mchezo kati yao na Gor Mahia ya Kenya, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam leo.
Mgeni rasmi katika mchezo wa fainali za Kombe la Kagame kati ya Azam FC na Gor Mahia, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Saidi Sadiki, akisalimiana na waamuzi wa mchezo wa fainali kati ya Azam FC na Gor Mahia ya Kenya, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam leo. 
Mgeni rasmi katika mchezo wa fainali za Kombe la Kagame kati ya Azam FC na Gor Mahia, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Saidi Sadiki, akisalimiana na kukagua timu ya Gor Mahia ya Kenya, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam leo. 
Wachezaji wa timu za Azam FC na Gor Mahia ya Kenya, wakisalimiana kabla ya mchezo wa fainali kati yao, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam leo.
Mgeni rasmi katika mchezo wa fainali za Kombe la Kagame kati ya Azam FC na Gor Mahia, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Saidi Sadiki, akisalimiana na Kocha wa timu ya Gor Mahia ya Kenya, Frank Nuttal.
Wachezaji wa timu ya Gor Mahia wakipata picha ya pamoja kabla ya mchezo huo.
Mgeni rasmi katika mchezo wa fainali za Kombe la Kagame kati ya Azam FC na Gor Mahia, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Saidi Sadiki, akisalimiana na Kocha wa timu ya Azam FC, Stewart Hall  kabla ya mchezo kati yao na Gor Mahia ya Kenya, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam leo. 
 Wachezaji wa timu ya Azam FC wakipata picha ya pamoja kabla ya mchezo huo. 
Mashabiki wa timu ya Simba, wakiwa kwenye jukwaa lao kwa ajili ya kufuatilia mchezo huo. 
Mashabiki wa Gor Mahia ya Kenya wakiwa kwenye jukwaa tayari kufuatilia mchezo kati ya timu yao na Azam FC ya Tanzania, Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam leo. 
 Ubao wa matokeo ukiwa 0-0 mara baada ya kuanza kwa mchezo huo.
Mashabiki wa Azam FC wakifuatilia mchezo huo. 
Haruna Shakava wa Gor Mahia akiondoa mpira huku akifuatwa na Kipre Tchetche wa Azam FC.
John Bocco wa Azam FC, akikimbia kushangilia baada ya kuipatia timu yake bao la kwanza katika mchezo huo.
John Bocco wa Azam FC, akiwa na wachezaji wenzake wakifurahia bao hilo, aliloifungia timu yake hiyo. 
Shah Farid Mussa wa Azam FC akiudhibiti mpira wa juu, huku akimwacha Harun Shakava wa Gor Mahia, akigagaa chini, wakati wa mchezo huo wa Fainali ya michuano ya Kombe la Kagame, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam leo. Azam FC wametwaa kombe la mashindano hayo kwa kuifunga Gor Mahia mabao 2-0. 
 Aucho Khalid wa Gor Mahia akiondoka na mpira huku akifuatwa na Kipre Tchetche wa Azam FC.
Ubao wa matokeo ukionesha Azam FC bao 1 na Gor Mahia 0. 
Wachezaji Sibomana Abouba (kushoto) na Haruna Shakava wote wa Gor Mahia wakiutuliza mpira huku Agrey Moris akiufuata.
John Bocco wa Azam FC akimtoka Mussa Mohammed wa Gor Mahia. 
John Bocco wa Azam FC akipambana na Mussa Mohammed wa Gor Mahia kuwania mpira.  
Wachezaji wa Azam FC, wakishangilia bao la pili la timu hiyo, lililofungwa na Kipre Tchetche. 
Ubao wa matokeo ukionesha Azam FC mabao 2 na Gor Mahia 0. 
 Mashabiki wa Azam FC, wakishangilia timu yao hiyo.
Mwisho wa mchezo wachezaji wa Azam FC, wakikimbia na kwenda kwenye majukwaa mbalimbali kuwashukuru watazamaji waliokuwa wakiwashangilia katika mchezo huo. 
Mgeni rasmi, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Saidi Sadik (kushoto) na Waziri Mkuu mstaafu wa Kenya, Raila Odinga (katikati), wakiwavisha medali wachezaji wa Gor Mahia ya Kenya.   
Mgeni rasmi, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Saidi Sadik (kushoto) na Waziri Mkuu mstaafu wa Kenya, Raila Odinga (katikati), wakiwavisha medali wachezaji wa Azam FC.  
Balozi wa Rwanda nchini Tanzania, Eugene Kayihura, akimkabidhi dola 10,000 Nahodha wa KCCA ya Uganda baada ya timu yake kushika nafasi ya Tatu katika mashindano hayo. 
Balozi wa Rwanda nchini Tanzania, Eugene Kayihura, akimkabidhi dola 20,000 Nahodha wa wa Gor Mahia baada ya kuibuka na ushindi wa Pili wa mashindano hayo.
Balozi wa Rwanda nchini Tanzania, Eugene Kayihura, akimkabidhi dola 30,000 Nahodha wa Azam FC, John Bocco mara baada ya timu yake hiyo kuibwaga Gor Mahia ya Kenya mabao 2-0 katika mchezo huo wa fainali.
Mgeni rasmi, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Saidi Sadik (kushoto), akimkabidhi Nahodha wa timu ya  Azam FC, John Bocco, Kombe la Ubingwa wa mashindano ya Kagame, baada ya kuifunga Gor Mahia ya Kenya mabao 2-0, katika mchezo wa fainali, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam leo. Pamoja na kutwaa kombe hilo pia wamekabidhiwa kitita cha dola 30,000. Kushoto ni Rais wa Shirikisho la Soka Afrika Mashariki na Kati (CECAFA), Leodger Tenga na wapili kulia ni Waziri Mkuu mstaafu wa Kenya, Raila Odinga. 
Mgeni rasmi, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Saidi Sadik (kushoto), akimkabidhi Nahodha wa timu ya  Azam FC, John Bocco, Kombe la Ubingwa wa mashindano ya Kagame, baada ya kuifunga Gor Mahia ya Kenya mabao 2-0, katika mchezo wa fainali, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam leo. Pamoja na kutwaa kombe hilo pia wamekabidhiwa kitita cha dola 30,000. Wa pili kulia ni Waziri Mkuu mstaafu wa Kenya, Raila Odinga. 
Mgeni rasmi, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Saidi Sadik (kushoto), akimkabidhi Nahodha wa timu ya  Azam FC, John Bocco, Kombe la Ubingwa wa mashindano ya Kagame, baada ya kuifunga Gor Mahia ya Kenya mabao 2-0, katika mchezo wa fainali, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam leo. Pamoja na kutwaa kombe hilo, pia wamekabidhiwa kitita cha dola 30,000. Kushoto ni Rais wa Shirikisho la Soka Afrika Mashariki na Kati (CECAFA), Leodger Tenga, Waziri Mkuu mstaafu wa Kenya, Raila Odinga (wa tatu kulia) na wa kwanza ni Balozi wa Rwanda nchini Tanzania, Eugene Kayihura.
Wachezaji wa Azam FC wakishangilia mara baada ya kukabidhiwa Kombe la Ubingwa wa michuano ya Kombe la Kagamena Mgeni rasmi, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Saidi Sadik, Uwanja wa Taifa jijini leo.

No comments