Obama kutembele kijiji alichozaliwa baba yake nchini Kenya
Maandishi yanayosomeka, Obama in Kenya ndiyo yanayotawala mitandao ya kijamii nchini Kenya, huku rais huyo akitarajiwa kulitembelea taifa hilo alilozaliwa na kukulia baba yake.
Hata hivyo, wakanakijiji wa kijiji cha Kogelo
ambapo babaake Obama alizaliwa na kulelewa sasa hawatalazimika kufanya
maandalizi ya aina yoyote kufuatia ziara hiyo baada ya balozi wa
Marekani nchini Kenya Robert Godec kusema kuwa rais huyo hatozuru kijiji
cha Kogelo.
''Ana mda mchache sana kwa hivyo basi atakuwa Nairobi pekee'', alisema bwana Godec akizungumza na runinga ya KTN.
No comments