Bonanza la Ali Kiba kugonga nyoyo za mashabiki wa TMK wiki ijayo
![]() |
Ali Kiba |
Mwanamuziki nyota wa kizazi kipya, Ali Kiba 'Alikiba' wa jijini Dar es Salaam, atajitupa jukwaani kuwapa raha ya vigongo vyake mashabiki wa muziki huo katika bonanza maalumu la kumuenzi mwanamuziki huyo 'Timu Kiba Day' lililoandaliwa na wadau wake,litafanyika mwishoni mwa wiki ijayo.
Akitoa taarifa hiyo, Dar es Salaam, Mwenyekiti wa bonanza hilo, Omary Kombe, amesema bonanza hilo ni maalumu kwa mashabiki na wapenzi wa muziki wa msanii huyo ambaye wanatarajia atakuwepo kushuhudia na kutoa burudani.
Anasema bonanza hilo linatarajiwa kuanza Agosti 8 na kumalizika Agosti 9, mwaka huu ambalo litahusisha michezo mbalimbali ikiwemo mpira wa miguu.
"Wadau wote wa Alikiba Wilaya ya Temeke tutakuwepo kwenye bonanza hilo ambapo zawadi mbalimbali kwa washiriki zitatolewa sambamba na burudani kutoka kwa msanii wetu ambayo itakuwa mahususi kwa mashabiki wake," anasema.
All that considered frontal cortex blowing subject, all around touchy signs are I was unable to say whether they are just reasonable as astounding as your work out. Wikipedia account registration guide
ReplyDelete