Simba yaikandamiza KMKM 3-1
Na Frank Balile
KMKM ya Zanzibar, ambayo ilikuwa jijini hapa kwa mechi mbili za kirafiki za kuwaweka sawa watani wa jadi, Simba na Yanga, kabla ya kuumana katika mechi yao Nani Mtani Jembe itakayopigwa Desemba 21, mwaka huu Uwanja wa Taifa, baada ya kuchapwa mabao 3-1 dhidi ya Simba.
Katika mechi yake ya kwanza iliyopigwa jana, KMKM ilikubali tena mabao 3-2, lakini wakinufaika na ufundi wa makocha wawili wa kigeni.
KMKM inafundishwa na mzawa Ali Bushiri, ilionesha soka zuri, ingawa walikosa vitu vichache sana hasa safu yake ya kiungo.
Simba walijipatia mabao yao kupitia kwa Said Ndemla dakika ya 11 na bao la pili likiwekwa wavuni na Edward Christopher dakika ya 16.
KMKM waliingia kipindi cha pili kwa nguvu na kufanikiwa kupata bao lao dakika ya 71, likiwekwa wavuni na Ally Ahmed ‘Shiboli’ kwa mkwaju wa penalti, kufuatia beki Salum Omar kumchezea vibaya Juma Mbwana.
Dakika ya 89, Simba iliongeza bao la tatu lililowamaliza nguvu KMKM, lililofungwa na Henry Joseph kwa penalti, kufuatia Issa Abdallah kuangushwa ndani ya eneo la hatari na mwamuzi Kenedy Mapunda kuamuru ipigwe penalti.
Kilichobaki sasa ni kwa watani wa jadi, Simba na Yanga kuumana Desemba 21, katika mchezo wa Nani Mtani Jembe, ulioandaliwa na wadhamini wa timu hiyo, Kampuni ya Bia Tanzania (TBL).
Simba: Yaw Berko, Haruna Shamte, Omary Salum, Henry Joseph, Joseph Owino, Jonas Mkude, Uhuru Seleiman, Said Ndemla/Ramadhan Kipalamoto, Edward Christopher/William Lucian, Betram Mwombeki/Tambwe/Issa Abdallah na Issa Rashid ‘Baba Ubaya’.
KMKM: Mudathir Khamis, Kassim Nemshi, Faki Ali, Khamis Ali, Iddi Mgeni/mudrik abdallah, Ibrahim Khamis/makame nuhu, Nassor Ally, Juma Mbwana, Hadji Simba, Ali Ahmed ‘Shiboli’ na Maulid Kapenta/Khalid khamis.

No comments