Header Ads

ad

Breaking News

Liverpool yaiua Tottenham 5-0

MPACHIKA mabao mtukutu wa Liverpool, Luis Suarez, amezidi kuonesha makali yake kwa kucheka na nyavu, baada ya kutupia mabao mawili kati ya matano yaliyofungwa dhidi ya Tottenham Hotspur katika Ligi Kuu ya England. 
 
Suarez alifunga aliifungia Liverpool bao la kwanza dakika za 18, kabla ya Henderson kuongeza la pili dakika ya 40, huku Flanagan akiongeza la pili dakika ya 75, Suarez aliongeza bao la nne dakika ya 84 na Sterling akamalizia bao la tano dakika ya 89.
Kwa mara ya kwanza akiiongoza timu hiyo kama nahodha, baada ya Steven Gerrard kuwa benchi kwa maumivu, Suarez alionesha uwezo mkubwa uwanjani na kumtumia salama kocha wake kuwa, anaweza kuwa kiongozi wa wenzake uwanjani.
Luis Suarez, akishangilia bao lake la kwanza.
                             Prolific: The skipper scored his 16th Premier League goal of the season
Nahodha Luis Suarez akishangilia bao lake lingine
 
Katika mechi nyingine ya Ligi ya England, Manchester United imeona mwezi baada ya kuichapa Atson Villa mabao 3-0, katika mechi iliyopigwa nchini humo.
Bao la kwanza la Man United lilifungwa na Danny Welbeck dakika ya 15 na bao la pili dakika ya 17, kabla ya Tom Cleverley kupiga bao la tatu dakika ya 52.
Man United wanaofundishwa na Kocha David Moyes, ilishuka uwanjani ikiwa na kumbukumbu mbaya ya kuchapwa mechi tatu mfululizo.
 
Tom Cleverley akifunga bao la tatu kwa Man United dhidi ya Aston Villa

No comments