Bafana Bafana yaiduwaza Hispania, yaichapa bao 1-0
Afrika Kusini 'Bafana Bafana' imefanya mambo ya ajabu, baada ya kuibuka na ushindi
wa bao 1-0 dhidi ya Hispania, katika mchezo wa kirafiki
uliochezwa nchini Afrika Kusini.
Bao pekee lililowapa raha Waafrika Kusini lilifungwa na Bernard
Parker dakika ya 56, lililokamilisha furaha yao, hasa kwa kuwafunga mabingwa wa Kombe la Dunia na Ulaya, Hispania.
Katika mchezo mwingine wa kirafiki wa kimataifa
uliozikutanisha timu za Ujerumani na England uliochezwa kwenye Uwanja wa
Wembley ulimaliza kwa Three Lions kushindwa kulipa kisasi na kukubali kipigo
cha bao 1-0.
England na Ujerumani walikutana kwa mara mwisho
mwaka 2010 kwenye fainali za Kombe la Dunia na kukubali kipigo cha mabao 4-1
katika hatua ya robo fainali na kuyaaga mashindano hayo.
Bao pekee katika mchezo huo lilifungwa na beki wa Arsenal Per Martesacker katika ya 39 na kufanikiwa kudumu hadi mwisho wa mchezo huo.
No comments