Header Ads

ad

Breaking News

Serengeti Boys yaalikwa Olimpiki Afrika Kusini

Timu ya Taifa ya Tanzania kwa vijana wenye umri chini ya miaka 20
(Serengeti Boys) imealikwa kushiriki Olimpiki ya Afrika itakayofanyika
Mei mwakani.

Mpira wa miguu ni kati ya michezo 22 itakayoshindaniwa katika
mashindano yatakayofanyika Gaborone, Botswana chini ya Kamati za
Olimpiki za Afrika (ANOCA).

Kwa mujibu wa Kamati ya Olimpiki ya Tanzania (TOC), Tanzania
imepewa nafasi ya kushiriki katika michezo hiyo ya Olimpiki kwa Afrika
kutokana na kuwa na programu nzuri za vijana hasa chini ya umri wa
miaka 17.

Hiyo itakuwa ni michezo ya Pili ya Afrika kwa Olimpiki ambapo ya
Kwanza ilifanyika mwaka 2010 jijini Rabat, Morocco.

No comments