Header Ads

ad

Breaking News

Bendi mpya ya Malaika yarekodi mbili mpya


Christian Bella
Na Mwandishi Wetu
BENDI mpya ya muziki wa dansi, Malaika Music, itazinduliwa Novemba 15, mwaka huu katika ukumbi wa Mzalendo Pub, uliopo Kijitonyama jijini Dar es Salaam.
Akizungumza jijini Dar es Salaam jana, Katibu wa bendi hiyo, Andrew Sekedia, alisema tayari wamerekodi nyimbo mbili na moja ikiwa kwenye video.
Sekedia ambaye aliwahi kutamba katika Kampuni ya African Stars Entertainment Tanzania (ASET), wakati huo ilikuwa ikimiliki bendi mbili, African Revolution 'Tam Tam' na African Stars 'Twanga Pepeta', kabla ya kuhamia

Akudo Impact, alisema ujio wa bendi hiyo ni kutaka kuongeza changamoto katika muziki huo.
"Wote tuliopo katika bendi hii ya Malaika, tumefanya kazi na bendi nyingi, naweza kusema tumekamilika, hivyo tutahakikisha tunafanya vizuri katika ushindi," alisema.

Sekedia alizitaja nyimbo walizorekodi ni 'Nakuhitaji' na 'Mtu wa Watu', lakini tayari wakiwa wameandaa nyimbo zaidi 10.
Sekedia alisema kuwa, wataanza kufanya maonesho rasmi baada ya uzinduzi wa bendi hiyo mwezi ujao, ambapo watakuwa na siku maalumu.
Bendi hiyo ili chini ya Mfalme wake, Christian Bella 'Obama', ilianza kambi jijini Dar es Salaam mwezi uliopita, tayari imetunga nyimbo zaidi ya sita, lakini wamekamilisha kurekodi mbili.

No comments