Header Ads

ad

Breaking News

Arsenal yalala, Chelsea yapeta Ulaya

Giroud sakifunga bao dhidi yaBorussia Dortmund
LONDON, England
ROBERT Lewandowski, aliwakatisha tamaa Arsenal baada ya kuiwezesha timu yake ya Borussia Dortmund kuibuka na ushindi wa mabao 2-1, katika mechi ya Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya iliyopigwa kwenye Uwanja wa Emerates, London.

Dortmund walipata bao la kwanza, baada ya kutumia viuzri makosa ya Aaron Ramsey nje kidogo ya eneo la hatari, huku Lewandowski akimtengenezea pasi nzuri Henrik Mkhitaryan, aliyeukwamisha mpira wavuni.

Lakini, Olivier Giroud, aliisawazishia Arsenal bao, akitumia vizuri mpira wa krosi uliopigwa na Bacary Sagna.

Dakika nane kabla ya mchezo kumalizika, Dortmund walijiaptia bao la ushindi kupitia kwa Lewandowski, aliyetumia vizuri pasi kutoka kwa Kevin Grosskreutz.

Mabao mawili ya Fernando Torres, yaliisaidia Chelsea kuibuka na ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Schalke, katika mechi ya Kundi E.

Torres aliifungia Chelsea bao la kwanza dakika ya tano akiunganisha mpira wa kona uliopigwa na Branislav Ivanovic. Bao lake la pili la Torres,baada ya Eden Hazard na Oscar kuonana vizuri kabla ya mfungaji huyo kuukwamisha mpira wavuni.

AC Milan na Barcelona, ziligawana pointi baada ya kushindwa kutambiana katika mchezo wao uliopigwa kwenye Uwanja wa San Siro.

Milan walijiaptai bao lao dakika ya 10, wakati Robinho alipofanikiwa kumiliki mpira na kutoa pasi kwa Kaka, kabla ya kuukwamisha mpira wavuni.

Lakini, Lionel Messi aliisawazishia timu yake bao, muda mfupi tu. Timu zote mbili zilishambuliaji kwa zamu, lakini zilishindwa kuongeza mabao mengine.

Celtic iliwaduwaza Ajax mjini Glasgow, kwa kuwafunga mabao 2-1, wakijiweka katika nafasi nzuri baada ya matokeo ya sare kati ya Milan na Barca, mechi hizo za Kundi H.

James Forrest aliifungia timu yake bao la kwanza kwa mkwaju wa penalti, baada ya Stefano Denswil kumchezea vibaya Anthony Stokes.

Atletico Madrid iliibuka na ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Austria Vienna, katika mchezo uliopigwa kwenye Uwanja wa Franz Horr.

Atletico ilipata mabao yake mawili ndani ya dakika 20 za kwanza mjini Vienna, pasi ya Koke ilimkuta Filipe Luis akiwa sehemu nzuri na kuutumbukiza mpira wavuni.

Dakika 12 baadaye, Diego Costa aliiongezea Atletico bao la pili na tatu akifunga kwa kuitumia vizuri krosi ya Emiliano Insuas.

Napoli iliibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Marseille.

Jose Maria Callejon aliifungia timu hiyo kutoka Italia bao, huku Duvan Zapata akiongeza bao la pili, kabla ya Jordan kuifungia timu yake bao.

Porto ililala bao 1-0 dhidi ya Zenit St Petersburg, bao pekee likifungwa na Alexander Kerzhakov.

Bao la kusawazisha lililofungwa dakika za mwisho na Leandro Tatu, liliiwezesha timu yake ya Steaua Bucuresti kutoka sare ya bao 1-1 dhidi ya FC Basel nchini  Romania.

Kevin-Prince Boateng wa Schalke na John Terry wa Chelsea, wakiwania mpira wakati wa mechi yao. Chelsea ilishinda mabao 3-0.

No comments