Micho aomba kazi Harambee Stars
![]() |
Micho |
KOCHA
wa timu ya taifa ya Rwanda, Milutin Sredojevic ‘Micho’, anaitamani timu ya
taifa ya Kenya ‘Harambee Stars’ kuifundisha.
Supersport.com
limepata taarifa kwamba, Micho, Kocha wa Uganda ‘The Cranes’, Bobby Williamson na kocha wa zamani wa
Burundi, Adel Amrouche, ni miongoni mwa makocha wanaotajwa nchini Kenya.
“Ninaweza
kuthibtihsa kuwa, Micho, Amrouche na Williamson, wameeleza nia yao. Wametuma
maombi ya kazi hiyo,” mtoa habari aliiambia supersport.com.
Kocha
wa zamani wa El Mereikh, 'Micho' alihudhuria kwenye Uwanja wa Nyayao wakati
Kenya ilipocheza na Burundi, katika mechi ya kuwania kufuzu fainali za Mataifa
ya Afrika kwa wachezaji wanaocheza ligi ya ndani (CHAN), kitu kilichotoa uvumi.
Pia,
Amrouche yupo nchini Kenya, inawezekana kwa mazungumzo na Shirikisho la Soka
Kenya.
Kenya
hawana kocha mpaka sasa, baada ya Mfaransa Henri Michel, kuachia ngazi, baada
ya kucheza mechi mbili za kirafiki na kuchapwa na timu za taifa za Afrika
Kusini na Tanzania.
Awali,
Kocha wa zamani wa Nigeria ‘Super Eagles’,
Samson Siasia, alikuwa akihusisha na kazi hiyo.
Harambee
Stars itakwenda nchini Libya Jumamosi, ikiwa na wachezaji wake nyota wanaocheza
nje, akiwemo Victor Wanyama, Arnold Origi, Ayub Timbe na Dennis Oliech.
No comments