Mariga alamba fomu Parma kwa mkopo
![]() |
Mariga |
KIUNGO
wa timu ya Inter Milan ya Italia, MacDonald Mariga, amejiunga na klabu yake ya
zamani ya Parma kwa mkopo mpaka mwishoni mwa msimu.
Kwa
mujibu wa taarifa za mtu wa karibu na mchezaji huyo, Mariga aliamua kukimbilia Parma ili aweze
kupata nafasi ya kucheza mara kwa mara katika kikosi cha kwanza.
“Siwezi
kuthibitisha kwamba, Mariga amejiunga Parma kwa mkopo.”
Taarifa
zilizonukuliwa na vyombop vya habari vya Italia, vimesema mchezaji huyo alitoa
sababu ya kuondoka mInter Milan.
"Ninakwenda
Parma, pale ni nyumbani. Sikupata nafasi ya kucheza, sina nafasi,” alinukuliwa
na mtandao wa Inter.
Reading
FC waliripotiwa kutaka kumsajili miaka mitatu iliyopita, wakati akielekea kutua
Manchester City.
Mariga
ni mchezaji pekee kutoka Afrika Mashariki aliyefanikiwa kulibeba kombe la Ligi
Kuu Italia ‘Serie A’ na Klabu Bingwa Ulaya.
No comments