KIM ATEUA 21 STARS WA KUIVAA CAMEROON
![]() |
Kim Poulsen |
Akizungumza
na Waandishi wa Habari, Dar es Salaam leo (Januari 31 mwaka huu), Kim amesema
mechi dhidi ya Cameroon itakuwa kipimo kizuri kwake kwa sababu ni sehemu ya
maandalizi kabla ya kucheza mechi ya mchujo ya Kombe la Dunia dhidi ya Morocco
itakayofanyika Machi mwaka huu.
“Itakuwa
mechi ngumu na kipimo sahihi kwetu. Tuko tayari, tutacheza kwa staili yetu kwa
sababu ni sehemu ya maandalizi kabla ya mechi dhidi ya Morocco. Ni mechi nzuri
kwa sababu wachezaji wameonyesha wako tayari.
“Tumetoka
kucheza dhidi ya Zambia na Ethiopia. Lengo ni Taifa Stars kucheza fainali za
AFCON 2015, kwa hiyo mechi dhidi ya Cameroon ni sehemu ya mipango yetu
kuhakikisha tunafika huko,” amesema Kim ambaye amerejea nchini juzi kutoka
Afrika Kusini kuzifuatilia timu za Morocco na Ivory Coast zilizo kundi moja na
Tanzania katika mechi za mchujo za Kombe la Dunia.
Taifa
Stars inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager itacheza na Morocco, Machi 24
mwaka huu Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. Stars inashika nafasi ya pili katika
kundi lake nyuma ya Ivory Coast inayoongoza. Timu nyingine katika kundi hilo ni
Gambia.
Wachezaji
aliowaita kwenye kikosi chake ni makipa Juma Kaseja (Simba), Mwadini Ali (Azam)
na Aishi Manula (Azam). Mabeki ni Erasto Nyoni (Azam), Nassoro Cholo (Simba),
Aggrey Morris (Azam), Nadir Haroub (Yanga), Kelvin Yondani (Yanga), Shomari
Kapombe (Simba) na Issa Rashid (Mtibwa Sugar).
Viungo
ni Amri Kiemba (Simba), Simon Msuva (Yanga), Frank Domayo (Yanga), Shabani
Nditi (Mtibwa Sugar), Salum Abubakar (Azam), Khamis Mcha (Azam), Athuman Idd
(Yanga) na Mwinyi Kazimoto (Simba). Washambuliaji ni Mrisho Ngasa (Simba), na
Mbwana Samata na Thomas Ulimwengu wanaochezea timu ya TP Mazembe ya Jamhuri ya
Kidemokrasi ya Congo (DRC).
Boniface
WamburaOfisa Habari
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)
No comments