Kamati ya uchaguzi TFF yapitisha wagombea wote
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
MAAMUZI KUHUSU PINGAMIZI DHIDI YA
WAOMBAJI UONGOZI
WA TFF NA TPL BOARD
31 JANUARI 2013
Kamati ya Uchaguzi ya TFF kwa kuzingatia
Kanuni za Uchaguzi za TFF Ibara ya 11(4) katika kikao chake kilichofanyika
tarehe 30 Januari 2013, ilijadili pingamizi zilizowekwa dhidi waombaji uongozi
wa TFF na TPL Board na kutoa maamuzi kama ifuatavyo:
1.
Waombaji uongozi wa TPL Board
(a)
Pingamizi
dhidi ya Ndg. Said Muhammed Abeid anayeomba kugombea nafasi ya
Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya Ligi (TPL Board): Kamati ilijadili
pingamizi iliyowasilishwa na Ndg. Frank M. Mchaki dhidi ya Ndg. Said
Muhammed, aliyeoomba Kamati ya Uchaguzi ya TFF kumwondoa mwombaji uongozi
kugombea nafasi aliyoomba, kwamba Ndg. Said Muhammed:
(i)
Si Mwenyekiti wa Klabu ya Azam na hivyo hana sifa za kugombea uongozi wa TPL
Board.
(ii)
Si mkweli katika maelezo aliyoyatoa kwenye fomu yake ya maombi ya uongozi.
Kamati
ya Uchaguzi ya TFF ilipitia maelezo ya Mweka pingamizi na ilijiridhisha kuwa
pingamizi iliyowasilishwa mbele yake na Ndg. Mchaki haikukidhi matakwa Kanuni
za Uchaguzi za TFF Ibara ya 11(2) kwa kuwa haikuambatanishwa na vielelezo
vyovyote kuthibitisha maelezo ya pingamizi. Kamati ya Uchaguzi ya TFF
imeitupa pingamizi hiyo.
(b)
Pingamizi
dhidi ya Ndg. Yusufali Manji anayeomba kugombea nafasi ya Mwenyekiti wa
Bodi ya Ligi (TPL Board): Kamati ilijadili pingamizi zilizowasilishwa na Ndg.
Daniel T. Kamna na Ndg. Juma Ally Magoma walioomba Kamati ya Uchaguzi ya TFF
kumwondoa mwombaji uongozi kugombea nafasi aliyoomba, kwamba Ndg. Yusufali
Manji :
(i)
Hana uzoefu wa uendeshaji wa Mpira wa Miguu uliothibitishwa wa angalau miaka
mitano (5) wa uendeshaji wa mpira wa miguu.
(ii)
Hana sifa ya kuwa ama mchezaji Mpira wa Miguu, Kocha, Mwamuzi au kushiriki katika
uendeshaji wa Mpira wa Miguu katika ngazi ya Mkoa au Ligi daraja la kwanza.
(iii)
Hana elimu ya kidato cha nne
(iv)
Ameshindwa kusimamia katiba ya Young Africans Sports Club Ibara ya 10(6),
18(1)b, 27 (2) na (5).
Kamati
ya Uchaguzi ya TFF ilipitia pingamizi hizo na ilijiridhisha kuwa pingamizi
zilizowasilishwa mbele yake na Ndg. Daniel T. Kamna na Ndg. Juma Ally Magoma
hazikukidhi matakwa Kanuni za Uchaguzi za TFF Ibara ya 11(2) kwa kuwa
hazikuambatanishwa na vielelezo vyovyote kuthibitisha maelezo ya pingamizi.
Kamati ya Uchaguzi ya TFF imezitupa pingamizi hizo.
(c)
Pingamizi
dhidi ya Ndg. Hamad Yahya Juma anayeomba kugombea nafasi ya Mwenyekiti
wa Bodi ya Ligi (TPL Board): Kamati ilijadili pingamizi iliyowasilishwa na Ndg.
Frank M. Mchaki dhidi ya Ndg. Hamad Yahya Juma, kwamba Ndg. Hamad Yahya
Juma:
(i)
Si Mwenyekiti wa Klabu ya Mtibwa na hivyo hana sifa za kugombea uongozi wa TPL
Board.
(ii)
Si mkweli na mwadilifu na amekuwa akijipachika cheo cha mwenyekiti wa klabu.
Kamati
ya Uchaguzi ya TFF imeitupa pingamizi ya Ndg. Frank M. Mchaki kwa
kuwa pingamizi iliyowasilishwa mbele yake haikukidhi matakwa ya Kanuni za
Uchaguzi za TFF Ibara ya 11(2) kwa kutoambatanishwa na vielelezo vyovyote
kuthibitisha maelezo ya pingamizi.
2.
Waombaji uongozi wa TFF
(a)
Pingamizi
dhidi ya Ndg. Athumani K. Kambi anayeomba kugombea nafasi ya Mjumbe wa
Kamati ya Utendaji ya TFF kupitia Kanda ya 9 (Mtwara na Lindi): Ndg. Kambi
aliwekewa pingamizi kwamba amefanya Kampeni kabla ya muda uliopangwa.
Kamati
imeitupa pingamizi ya Ndg. Jeremiah John Wambura kwa kuwa mweka
pingamizi hakutokea wakati alipotakiwa kufika kwenye Kamati ya Uchaguzi kutoa
utetetezi wake kuhusu pingamizi.
(b)
Pingamizi
dhidi ya Ndg. Eliud P. Mvella anayeomba kugombea nafasi ya Mjumbe wa
Kamati ya Utendaji ya TFF kupitia Kanda ya 7 (Iringa na Mbeya): Ndg. Mvella
aliwekewa pingamizi na Ndg. Said Kiponza, Ndg. Abu Changawa na Ndg. Peter
Naminga, kwamba Ndg. Mvella:
(i)
Akiwa mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya TFF kupitia Kanda hiyo ameshindwa kuleta
maendeleo ya soka katika ukanda huo.
(j)
Ana kesi ya rushwa katika mahakama ya wilaya ya Iringa
Kamati
imeitupa pingamizi hiyo kwa kuwa haikukidhi matakwa ya Kanuni za
Uchaguzi za TFF Ibara ya 11(2) kwa kutoambatanishwa na vielelezo vyovyote
kuthibitisha maelezo ya pingamizi.
(c)
Pingamizi
dhidi ya Ndg. Epaphra Swai anayeomba kugombea nafasi ya Mjumbe wa Kamati
ya Utendaji ya TFF kupitia Kanda ya 3 (Shinyanga na Simiyu): Kamati ilijadili
pingamizi zilizowasilishwa na Ndg. Ramadhani Sesso na Ndg. Tsotsie Chalamila,
kwamba Ndg. Epaphra Swai:
(i)
Alifanya ubadhilifu wa fedha alipokuwa Katibu wa Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa
wa Mwanza (MZFA).
(ii)
Alitumia madaraka yake vibaya alipokuwa MZFA kujinufaisha kwa kutumia MZFA.
(iii)
Alivunja Katiba ya MZFA na FIFA
(iv)
Anavuruga shughuli za uendeshaji mpira wa miguu mkoani Simiyu.
Kamati
ya Uchaguzi ya TFF ilipitia pingamizi hizo na ilijiridhisha kuwa wawekaji
pingamizi hawakuwa na sababu za msingi zilizoambatana na vielelezo
vinavyothibitisha maelezo ya pingamizi na kuwa pingamizi zilizowasilishwa mbele
yake zina chembechembe za wazi za mapatano ya hila na udanganyifu (collusion)
dhidi ya Ndg. Epaphra Swai. Kwa kutokidhi matakwa ya Kanuni za Uchaguzi za TFF
Ibara ya 11(2) na hila/udanganyifu kwa Kamati, Kamati ya Uchaguzi ya TFF imezitupa
pingamizi hizo.
(d)
Pingamizi
dhidi ya Ndg. Vedastus F.K Lufano na Ndg. Mugisha Galibona
wanaoomba kugombea nafasi ya Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya TFF kupitia Kanda
ya 2 (Mwanza na Mara): Ndg. Lufano na Ndg. Galibona waliwekewa pingamizi na Ndg.
Paul Mhangwa kwamba hawana uzoefu wa uendeshaji wa Mpira wa Miguu wa
miaka mitano (5).
Kamati
imeitupa pingamizi hiyo kwa kuwa haikuzingatia Kanuni za Uchaguzi
za TFF Ibara ya 11(2).
(e)
Pingamizi
dhidi ya Ndg. Michael R. Wambura anayeomba kugombea nafasi ya Makamu wa
Rais wa TFF: Pingamizi ziliwasilishwa na Ndg. Said Rubea Tamim na Ndg. Josea
Samuel Msengi kwamba Ndg. Wambura:
(i)
Alikiuka Katiba ya TFF kwa kuishitaki Klabu yake ya Simba mahakamani kuhusu
masuala ya uchaguzi.
(ii)
Alikosa uadilifu kwa kutumia kampuni yake binafsi kufanya biashara na Taasisi
aliyokuwa aniongoza akiwa Katibu Mkuu wa FAT.
(iii)
Amekuwa akijaribu kupotosha umma kwamba vyombo vya TFF havifanyi kazi zake kwa
kutumia haki na kuviita ‘Mahakama za Kangaroo (Kangaroo Courts).
(iv)
Mwaka 2004 alikiri kwamba alikuwa akiandikwa vizuri na vyombo vya habari kwa
kuwa alikuwa akivipa pesa na kwamba vyombo vya habari vilimgeuka kwa sababu
aliacha kuwapa waandishi pesa.
(v)
Mwaka 2004 alikataa kutekeleza maagizo ya FIFA ya kutaka nafasi ya Katibu Mkuu
wa FAT iwe ya kuajiliwa.
(vi)
Alikosa uwezo wa kutekeleza wajibu na malengo ya TFF.
Ndg.
Josea Samuel Msengi aliondoa pingamizi lake dhidi ya Ndg. Wambura. Kamati imelitupa
pingamizi la Ndg. Said Rubea Tamim kwa kuwa halikukidhi matakwa ya Kanuni
za Uchaguzi za TFF Ibara ya 11(2).
(f)
Pingamizi
dhidi ya Ndg. Jamal E. Malinzi anayeomba kugombea nafasi ya Rais wa TFF;
Aliwekewa Pingamizi na Ndg. Agape Fue kwamba:
(i)
Alivunja Katiba ya TFF kwa kufanya jitihada kubwa za kuhakikisha kuwa wanachama
wa TFF kikiwemo Chama chake cha Mkoa wa Kagera haviheshimu wala kutekeleza
maagizo ya TFF, CAF, CECAFA na FIFA baada ya Kamati ya Utendaji ya TFF
kuwasilisha mapendekezo ya mabadiliko ya Katiba kwa njia ya Waraka, ambayo
yalihusisha pia maagizo ya FIFA na CAF
(ii)
Hana sifa ya uzoefu wa miaka mitano katika uongozi wa mpira wa miguu.
(iii)
Anakosa uadilifu na haiba ya kuliwakilisha Shirikisho nje na ndani.
Kamati
imeitupa pingamizi ya Ndg. Agape Fue kwa kuwa mweka
pingamizi hakutokea wakati alipotakiwa kufika kwenye Kamati ya Uchaguzi kutoa
utetetezi wake kuhusu pingamizi hilo.
(g)
Pingamizi
dhidi ya Ndg. Athumani J. Nyamlani anayeomba kugombea nafasi ya Rais wa
TFF: Ndg. Nyamlani aliwekewa pingamizi na Ndg. Mintanga Yusuph Gacha na Ndg.
Medard Justiniani kwamba:
(i)
Ni Hakimu Mkazi katika Mahakama ya Tanzania na kwa maana hiyo ni mtumishi wa
umma hivyo alikosa kigezo na sifa ya kugombea nafasi ya urais wa TFF.
(ii)
Anakatazwa na Judicial Service Act, Public Service Act 2002 na Code
of Conduct for Judicial Officers of Tanzania kugombea nafasi aliyoomba ya
Rais wa TFF.
(iii)
Kutakuwa na Mgoganao wa kimaslahi endapo Ndg, Nyamlani atachaguliwa kuwa Rais
wa TFF.
(iv)
Amekosa umakini na uadilifu kwa kushindwa kutekeleza wajibu wake na kusababisha
Akanunti za TFF kufungiwa na TRA.
Ndg.
Mintanga Yusuph Gacha hakufika kutetea Pingamizi lake ni hivyo halikujadiliwa
na Kamati. Kamati imelitupa pingamizi la Ndg. Medard Justiniani kwa kuwa
alishindwa kuithibitishia Kamati kuwa alikuwa na ufahamu wa kutosha wa pingamizi
lake ikiwa ni pamoja na viambatanisho vyake, hali iliyotanabaisha kuwa
pingamizi hilo lilikuwa na chembechembe nyingi za hila na udanganyifu.
Angetile
Osiah
KATIBU
KAMATI
YA UCHAGUZI
No comments