Somalia yapata mwakilishi Miss East Africa 2012
![]() |
Halifa Ayan Yusuf |
PRESS RELEASE 30/10/2012
MISS EAST AFRICA 2012
Mrembo atakayeiwakilisha Somalia katika mashindano ya Miss East Africa mwaka huu ametangazwa rasmi
Mrembo huyo mwenye urefu wa futi 5.9 anaitwa HALIFA AYAN YUSUF aliyezaliwa Somalia Hargeisa na ana umri wa miaka 21.
Fainali za mashindano ya Miss East Africa 2012 zitafanjika tarehe 07 mwezi December mwaka huu katika ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es salaam ambapo zitashirikisha Nchi za Tanzania, Kenya, Uganda, Rwanda, Burundi, Somalia, Djibouti, Eritrea, Sudan, Ethiopia, Malawi, Madagascar, Reunion, Comoros, Seychelles, na Mauritius.
Mashindano ya Mwaka huu yanayosubiliwa kwa hamu yanatarajiwa kushuhudiwa na mamilioni ya watu Duniani kupitia kwenye luninga zao na pia kwa njia ya Internet ambapo yatautangaza utalii wa Tanzania kwa kiasi kikubwa na pia kujenga umoja wa Afrika mashariki na kudumisha utamaduni wa ukanda huu wa Afrika.
Mashindano ya Miss East Africa yanaandaliwa na kumilikiwa na kampuni ya Rena Events Ltd ya jijini Dar es salaam
Imeandikwa na kusainiwa na,
Rena Callist,
EXECUTIVE PRODUCER
MISS EAST AFRICA BEAUTY PAGEANT
Mobile: +255 755 755 755
No comments