Header Ads

ad

Breaking News

MECHI YA JKT RUVU, SIMBA YAINGIZA MIL 73/-

Msemaji TFF, Boniface Wambura
Mechi ya Ligi Kuu ya Vodacom kuwania ubingwa wa Tanzania Bara kati ya JKT Ruvu na Simba iliyochezwa jana (Septemba 19 mwaka huu) Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam imeingiza sh. 73,611,000.

Washabiki 12,884 walikata tiketi kushuhudia mechi hiyo ambapo viingilio vilikuwa sh. 5,000, sh. 8,000, sh. 15,000 na sh. 20,000. Kila timu ilipata sh. 16,154,161.02 wakati asilimia 18 ya Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) iliyokatwa ni sh. 11,228,796.61.

Mgawo mwingine umekwenda kwa msimamizi wa kituo sh. 20,000, posho ya kamishna wa mechi sh. 150,000, waamuzi sh. 70,000, mwamuzi wa akiba sh. 70,000, tiketi sh. 3,175,000, maandalizi ya uwanja (pitch preparation) sh. 400,000 na Wachina (stadium technical support) sh. 2,000,000.

Umeme sh. 300,000, ulinzi na usafi uwanjani sh. 2,350,000, Kamati ya Ligi sh. 5,384,720.34, Mfuko wa Maendeleo ya Mpira wa Miguu (FDF) sh. 3,230,832.20, uwanja sh. 5,384,720.34, Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA) sh. 1,076,944.07, Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Pwani (COREFA) sh. 1,076,944.07.

No comments