61 WASHUHUDIA MECHI YA AFRICAN LYON v POLISI MORO
Watazamaji
61 ndiyo waliokata tiketi kushuhudia mechi ya Ligi Kuu ya Vodacom kati ya
African Lyon na Polisi Moro iliyofanyika jana (Septemba 19 mwaka huu) Uwanja wa
Azam Complex, Dar es Salaam.
Mapato
yaliyopatikana katika mechi hiyo ambapo viingilio vilikuwa sh. 3,000 na sh.
5,000 ni sh. 185,000. Mgawo ulikuwa kama
ifuatavyo; kila timu sh. 20,287.91, asilimia 18 ya Kodi ya Ongezeko la Thamani
(VAT) sh. 27,457.62 na tiketi sh. 89,916.
Kamati
ya Ligi sh. 6,762.63, Mfuko wa Maendeleo ya Mpira wa Miguu (FDF) sh. 4,057.58,
Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar
es Salaam (DRFA) sh. 2,703.05, gharama za mchezo sh.
6,762.63 na uwanja sh. 6,762.63.

No comments