KLABU LIGI KUU, WADHAMINI VODACOM KUTETA
Klabu
za Ligi Kuu ya Vodacom zimekubaliana kukutana na mdhamini (kampuni ya simu za
mkononi ya Vodacom) kuzungumzia kipengele cha mkataba wa ligi hiyo kinachozuia
kampuni nyingine za mawasiliano kudhamini timu zinazocheza Ligi Kuu.
Maazimio
hayo yalifikiwa jana (Septemba 18 mwaka huu) katika kikao kati ya klabu hizo na
Kamati ya Ligi kilichofanyika ofisi za Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania
(TFF) chini ya Mwenyekiti wa Kamati hiyo Wallace Karia.
Wengine
waliohudhuria kikao hicho ni Katibu Mkuu wa TFF, Angetile Osiah na Ofisa Habari
wa TFF, Boniface Wambura.
Maazimio
mengine ya kikao hicho ni TFF kuiandikia barua African Lyon ambayo itaipeleka
kwa mdhamini wake (Zantel) ikielezea hatua hiyo ili kusimamisha udhamini huo
wakati ikisubiri matokeo ya mazungumzo kati ya klabu hizo na mdhamini wa Ligi
Kuu juu ya kipengele cha kuzuia washindani wa Vodacom.
Katika
mkutano huo, watendaji wawili wa Kamati ya Ligi ambayo iko katika kipindi cha
mpito kuelekea kuundwa kwa Bodi ya Ligi walitambulishwa kwa klabu hizo.
Watendaji hao ni Silas Mwakibinga ambaye ni Ofisa Mtendaji Mkuu (CEO) na Joel
Balisidya ambaye ni Ofisa wa Ligi (LO).
No comments