WACHEZAJI 11 KUTOKA NJE WAPATA ITC
![]() |
Yanga |
Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa
Miguu Tanzania (TFF) limepokea Hati ya Uhamisho wa Kimataifa (ITC) kwa
wachezaji 11 wa nje kati ya 14 walioombea usajili na klabu mbalimbali za Ligi
Kuu.
Wachezaji walioombewa usajili Yanga
na tayari ITC zao zimepatikana ni Nizar Khalfan kutoka Vancouver Whitecaps ya
Canada, Didier Kavumbagu (Atletico Olympic- Burundi) na Mbuyu Twite kutoka FC
Lupopo ya Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo (DRC).
Kwa upande wa Simba ni Musa Mude
(Sofapaka, Kenya) na Daniel Akuffor (Stella Abidjan, Ivory Coast) wakati Mtibwa
Sugar ni Shabani Kisiga timu ya El Itihad ya Oman.
Waliopata ITC kwa upande wa Kagera
Sugar ni Wilfred Ojodale Ame na Benjamin Efe Ofuyah wote kutoka FC Abuja ya
Nigeria. Wengine ni Deangelis Silva kutoka New Road ya Nepal kwenda Coastal
Union, George Odhiambo kutoka Randers FC ya Denmark kwenda Mtibwa Sugar na
Jerry Santo kutoka Tusker, Kenya kwenda Coastal Union.
Wachezaji ambao wameombewa usajili
na ITC zao bado hazijapatikana ni Salum Kinje na Pascal Ochieng wa AFC
Leopards, Kenya kwenda Simba na Ayoub Hassan Isiko kutoka Bull FC, Uganda
kwenda Mtibwa Sugar.
Bado klabu ambazo hazijakamilisha
usajili na kupata ITC zina fursa ya kufanya hivyo hadi Septemba 4 mwaka huu
ambapo dirisha litafungwa.
Pia TFF imetoa ITC kwa wachezaji
wanane walioombewa kwenda kucheza mpira wa miguu katika nchi za Kenya na
Msumbiji kutoka katika klabu mbalimbali za hapa nchini.
Wachezaji hao na klabu wanazokwenda
katika mabano ni Abdallah Ally Abdallah (CD Madchegde, Msumbiji), Almasi Khatib
Mkinda (Ferroviario da Beira, Msumbiji), David Naftali (Bandari, Kenya) na
Hassan Hassan Mustafa (CD Madchegde, Msumbiji).
Wengine ni Meshack Abel (Bandari,
Mombasa), Mohamed Banka (Bandari, Kenya), Thobias Davis Silas (CD Madchegde,
Msumbiji) na Thomas Maurice (Bandari, Kenya).
VIPIMO VYA TIBA KWA WACHEZAJI
Klabu zote zilizowasilisha
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) maombi ya usajili kwa wachezaji wao
zinatakiwa pia kuwasilisha nakala za hati zao za vipimo vya afya (medical
certificate) kwa mujibu wa kanuni za usajili.
No comments