Nyota wa NBA waendesha mafunzo ya kikapu Dar es salaam

Kutoka kushoto wachezaji nyota wa
mpira wa kikapu ktoka nchini Marekani Luol Deng wa Chicago Bulls’ ,
Phares Magesa Makamu Mwenyekiti TBF ,Amadou Makamu wa Rais wa NBA
Africa , na Mkurugenzi wa Ufundi wa NBA Kocha Jobby wakiwa katika
uwanja wa Julias Nyerere International Airport .
Nyota wa kikapu Luol Deng
wa Chicago Bulls na Hasheem Thabeet wa Oklahoma City Thunder wameendesha
mafunzo ya kikapu kwa vijana wadogo chini ys miaka 18.
Mafunzo hayo yalifanyika katika viwanja vya Don Bosco, ijumaa na jumamosi jiji Dar Es Salaam.
Pia mafunzo hayo yalihudhuriwa na
Makamu wa Rais wa NBA Afrika ndugu Amadou, Kocha wa NBA na Mkurugenzi
wa Ufundi wa NBA Afrika Jobby na Meneja Mkuu na Makamu wa Rais wa timu
ya Denver Nuggets ndugu Masai.
Ujio wa nyota hao na vigogo hao NBA ni faraja kubwa kwa kikapu Tanzania na ni matumaini yetu itakuwa ni chachu ya kukuza mchezo huo nchini.
Pia mazungumzo yalifanyika kati
ya viongozi wa TBF na NBA kuangalia namna ya NBA kusaidia kuendeleza
mchezo wa kikapu nchini na hususani katika maeneo ya miundombinu na
kusaidoa kujenga uwezo wa kiufundi kwa makocha wazalendo ili kuwa na
maendeleo endelevu katika kikapu.
Kwa niaba ya Shirikisho la mpira
wa kikaupu Tanzania tunawashukuru wachezaji hao na viongozi wote wa NBA
na tunaishukuru sana kampuni ya CocaCola kupitia kinywaji cha SPRITE kwa
kudhamini mafunzo hayo. www.fullshangwe.blogspot.com
No comments