MICHUANO YA KOMBE LA TAIFA 2012
![]() |
Ofisa Habari TFF, Boniface Wambura |
Michuano ya Kombe la Taifa (Taifa
Cup) inayoshirikisha kombaini za mikoa ya Tanzania Bara haitakuwepo mwaka huu
kutokana na kukosekana kwa udhamini.
Licha ya kukosekana kwa udhamini,
awali tulifikiria kuendesha mashindano hayo kwa michango ya wanachama wetu
(vyama vya mpira wa miguu vya mikoa) na Serikali za mikoa kugharamia timu zao.
Lakini baadhi ya wanachama wetu na
Serikali za mikoa walitushauri kuwa ni ngumu kuendesha mashindano hayo kwa sasa
kutokana na shughuli za kitaifa zinazoendelea hivi sasa ikiwemo maandalizi ya
sensa ya watu na makazi.
Kwa mujibu wa Kalenda ya Matukio ya
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), mashindano ya Kombe la Taifa
yalitakiwa kufanyika kuanzia Julai 23 hadi Agosti 6 mwaka huu.
Michuano ya Kombe la Taifa msimu
uliopita ilidhaminiwa na Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) kupitia bia ya
Kilimanjaro Premium Lager ambapo Mbeya iliibuka mabingwa katika fainali
iliyochezwa Uwanja wa Kumbukumbu ya Sheikh Kaluta Amri Abeid jijini Arusha.
No comments