Twite kuivaa Rayon akiwa na Yanga jijini Kigari
![]() |
Mbuyi Twite |
KIKOSI cha mabingwa wa Afrika Mashariki na Kati,
Yanga, kimekamilika baada ya beki wao mpya, Mbuyu Twite, kujiunga na wenzake
waliopo Kigali Rwanda, usiku wa kuamkia jana, akitokea kwao Lubumbashi (DRC).
Yanga wapo kwenye ziara jijini Kigali kwa mwaliko wa
Rais wa Rwanda, Paul Kagame, ambapo watakaa huko kwa siku saba.
Akizungumza leo, Mjumbe wa Kamati ya
Utendaji wa klabu hiyo, Abdallah Bin Kleb, alisema kwamba, Twite aliwasili saa
saba usiku na kujiunga kambini na jana asubuhi, alifanya mazoezi na wenzake
kwenye Uwanja wa Amahoro jijini Kigali.
“ Saa saba usiku wa kuamkia leo kwa saa za hapa Rwanda,
tulimpokea Twite akitokea kwao, Lubumbashi na asubuhi, amefanya mazoezi
na wenzake,” alisema Bin Klebu.
Ameongeza kuwa, baada ya chakula cha mchana hapo
jana, timu ilitarajiwa kukutana na Rais Kagame majira ya saa 9 alasiri.
Mbali na ujio wa Twite, kesho, Yanga watashuka dimbani
kuchuana na Rayon Sport, katika mchezo wa kirafiki, utakaopigwa Uwanja wa
Amahoro.
Jumamosi, wataendelea na mazoezi asubuhi na jioni,
kabla ya kuikabiri timu ya Polisi Jumapili, mechi ambayo itachezwa kwenye
Uwanja huo.
No comments