DSTV yapunguza gharama za kulipa
![]() |
Barbara Kambogi, Meneja Uhusiano MultiChoice Tanzania |
KATIKA
kuhakikisha DSTV inawakosha wapenzi wake katika matangazo yake ya moja
kwa moja ya mpira wa miguu wamepungaza gharama za kulipia ili kuwapa fursa
wadau wa soka kutumia king’amuzi hicho.
King’amuzi hicho cha DSTV kupitia kituo chake chake
SuperSport ndio kituo pekee kitakachoonesha ligi kuu ya England, Hispania ‘La
liga’, Italia Seria A, Ujerumani ‘Bundesliga’.
Mashindano mengine ambayo huoneshwa katika kituo cha
SuperSports ni Ligi ya Klabu Bingwa na Mataifa ya Ulaya.
Kwa upande wa Afrika, Super Sports inaonesha ligi ya
Afrika ya Kusini, Kenya, Uganda, Nigeria, Angola, Ghana, Zambia na mashindano
ya yanayosimamiwa na Shirikisho la Soka Afrika (CAF).
Hata hivyo, DSTV imeendelea kuonesha mechi za Kombe
la Dunia za wanawake wenye miaka chini
ya 20.
Super Spots kupitia king’amuzi chake cha DSTV, wamekuwa
wakirusha matangazo ya mechi moja kwa moja zaidi ya mechi 1,400 kwa mwaka.
Baadhi ya vipindi ambavyo vitakuwa vikirusha
matangazo hayo kuchambua soka ni Monday Night Football, EPL TV – Fan Zone, La
Liga Highlights Show, Simba Super
Soccer, Soccer Africa, Mpira Zambia na Naija.
No comments