Twite afufua 'sheshe' la Okwi
Emmanuel Okwi |
Na
Abdallah Mkwinda
KITENDO
cha Yanga kufanikiwa kumnasa mchezaji wa FC Lupopo ya DRC anayekipiga kwa mkopo
APR ya Rwanda, Mbuyi Twite, kimewashtua wapenzi wa Simba ambao wameanza kupata
hofu juu ya majaliwa ya mshambuliaji wao, Emmanueli Okwi.
Awali,
uongozi wa Simba ulijinadi kuwa ulishamalizana na Twite aliyeng’ara katika
michuano ya Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati iliyomalizika hivi karibuni
jijini Dar es Salaam akiwa na APR, lakini juzi ziliibuka taarifa za Yanga
kumnasa beki huyo kutokana na kazi nzuri iliyofanywa na mjumbe wa Kamati ya
Utendaji ya klabu hiyo, Abdallah Bin Kleb.
Mwenyekiti
wa Simba, Alhaji Ismail Aden Rage, aliwatangazia wanachama wa klabu yao katika
mkutano uliofanyika wiki iliyopita kuwa Twite ni mali yao na kwamba alitarajiwa
kutua jijini Dar es Salaam wakati wowote tayari kuitumikia klabu hiyo.
Lakini
kitendo cha Wekundu wa Msimbazi hao kuzidiwa kete kwa mchezaji huyo kama
SuperStar ilivyopasha juzi, wapenzi wa Simba sasa wamepatwa na mchecheto juu ya
Okwi wakihofu kuporwa na watani wao hao wa jadi.
Okwi,
ambaye aligonga kisiki katika majaribio nchini Australia, alirudi nchini kwao
Uganda alikokaa kwa siku chache kabla ya kutua jijini Dar es Salaam kwa ajili
ya tamasha la Simba, Simba Day lililofanyika Jumatano iliyopita kabla ya
kurejea kwao Uganda siku iliyofuata.
Kosa
walilofanya Simba Rwanda, linaweza kuendelekea tena Uganda ambapo baada ya
mabingwa hao wa ligi kushindwa kuweka
mambo sawa, Yanga wamekwenda huku kwa lengo la kumalizana naye.
Hali
hiyo ya Simba kushindwa kumalizana na Okwi,imepokelewa tofauti na
mashabiki na wanachama wa timu hiyo
,huku wakiutaka uongozi wafanye kila njia ili wahakikishe nyota huyo anabaki
Msimbazi.
“Hakutakuwa
na majadiliano kama Okwi akiondoka ,kwanini hawa viongozi wetu wanatufanyia
hivi ,hii ni timu ya wanachama sio ya kwao ,”hiyo ni kauli ya mwanachama wa
Simba.
Hatuwezi
kuvumilia ,viongozi wamezidi kutuongopea ,kwanza walituambia Twite anakuja
kumbe hakuna lolote na hili la Okwi ndio wanatupiga chenga,aliongeza mwanachama
huyo ,ambapo alitoa kauli hiyo juzi usiku katika makao makuu ya Simba.
Wakati
wa Simba ,ikishindwa kuongea na mchezaji huyo,viongozi wa Yanga wamelipokea
suala hilo kwa furaha ambapo timu hiyo inamuhitaji mchezaji huyo kwa udi na
uvumba.
Viongozi
hao wa Yanga, ambao waliweza kufanya nae mazungumzo mchezaji huyo akiwa Uganda
baada ya kurudi Australia ,sasa wameenda kumalizia picha hiyo ,ambapo mchezaji
huyo yupo nchini kwao katika kikosi chake cha Taifa.
Habari
ambazo Super Star ilizipata jana ni kwamba baada ya mchezaji huyo kumaliaza na
Yanga ,atakuja nchini na mwanasheria wake ili aweze kuvunja mkataba wake na Simba.
Miongoni
mwa sababu ambazo zinapelekea mchezaji huyo kusaka timu ya kuitumikia inatokana
na viongozi wa Simba kushindwa kumtimizia mahitaji yake ikiwa ni pamoja na
kumuongezea mshahara.
Mshambuliaji
huyo ,ambaye aliliambia Super Star,kuwa amebakiza mwaka mmoja wa kuitumikia
Simba lakini hayupo tayari kuongeza mkataba hadi pale
watakapozungumza makubaliano mapya.
Katika
mazungumzo hayo ,Okwi alikuwa anataka Dola za Marekani 80,000 kwa ajili ya
kuongeza mkataba pamoja mshahara dola 3,000 kwa mwezi zikiwa ni kama milioni 4
za Tanzania.
Baada
ya nyota huyo kutaka dau hilo viongozi wa Simba walionekana kutoafikiana na
msimamo wa mchezaji huyo.
Kitendo
cha kushindwa kupata majibu ya kuridhisha kwa nyota huyo wa Uganda juu ya
ongezeko lake la mshahara kitaweza kuigharimu Simba katika msimu ujao.
Kama
Yanga wakifanikiwa kupata saini ya mshambuliaji huyo watalazimika kumuacha
mchezaji wao mmoja wa kigeni kwa mujibu wa kanuni za Shiriko la soka
Tanzania(TFF).
Kanuni
za TFF,linazitaka timu ambazo zinashiriki ligi kuu kuwa na wachezaji watano na
sio vinginevyo.
No comments