Header Ads

ad

Breaking News

Ya Mbuyi Twite yametimia


Rais wa FC Lupopo, Victor Kasong, akihojiwa na TBC1, leo TFF

*Rais FC Lupopo, Katibu APR watia timu TFF kurudisha fedha za Simba

*Vigogo Wekundu wa Msimbazi wakwamisha zoezi, watofautiana


YAMETIMIA, yale yaliyokuwa yakiandikwa na gazeti hili la SuparStar, kwamba mchezji Mbuyi Twite, amekamilisha usajili wa kuwatumikia mabingwa wa soka Afrika Mashariki na Kati, yalitimia jana baada ya viongozi wa klabu za FC Lupopo ya DR Congo na APR ya Rwanda, kutua nchini kurudisha fedha za Simba.

Klabu ya Simba ilitangaza kumsajili beki huyo na kumtangaza wakati wa Simba Day kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, na kuonesha jezi namba nne atakayoitumia kwenye msimu ujao wa Ligi Kuu Tanzania Bara msimu ujao.

SuperStar iliandika katika toleo lake la juzi na jana kwamba, Twite ataitumikia Yanga msimu ujao, na hayo yalitimia jana baada ya Rais wa FC Lupopo, Victor Kasongo na Katibu Mkuu wa timu ya APR, ambaye hakutaka jina lake litajwe gazetini, kutua kwenye ofisi za Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), majira ya saa 11 jioni wakitaka kurejesha fedha za Simba walizompa mchezaji wao.

Akizungumza na SuperStar jana, Rais huyo wa FC Lupopo, Kasongo, muda mfupi kabla ya kuingia mitamboni, alisema kwamba, viongozi wa Simba walikurupuka kumsainisha beki huyo bila kuzungumza na uongozi wake.

“Tumekuja hapa TFF kurudisha fedha za Simba walizomsajili Twite, maana tumezungumza na viongozi wa klabu hiyo wanatoafutiana kauli zao, wengine wanasema tuchukue fedha, wengine wanakataa, tumeamua kuzileta hapa TFF, maana hapa ndio mwisho wa mambo yote,” alisema Kasongo.

“Tumekuja hapa TFF kurudisha fedha hizi baada ya kuona Simba wanachanganyana wenyewe, na hata kama TFF wakizikataa, nitarudi nazo DR Congo, watanifuata wenyewe, “ alisema.

Alisema kuwa, walikaa kwa muda mrefu katika ofisi za TFF wakiwasubiri viongozi wa Simba, lakini hawakutokea, hivyo watahakikisha wanazikabidhi TFF fedha zote.

Rais huyo wa FC Lupopo alisema kuwa, kama TFF nao wakikataa kuzipokea fedha hizo, watarudi nazo kwao DR Congo, hivyo Simba watakuwa na kibarua cha kuzifuata kwao.

“Twite alinifuata na kunieleza kwamba, Simba wananihonga fedha nyingi niende kwao, mimi kama mtu mkubwa na kiongozi wake, nikaona nimsaidie, kwanza hawa viongozi walifanya makosa makubwa kumsajili mchezaji bila kuzungumza na sisi viongozi, ni kinyume cha kanuni,” alisema.

Kasongo alisema kwamba, wameamua kurudisha fedha hizo ili kumuacha mchezaji wao awe huru na kama kuna timu inayomhitaji ifuate taratibu zinazotakiwa.

“Kwa hapa Tanzania, kama kuna timu yoyote inayomhitaji, viongozi wake tupo, waje tuzungumze na mambo yote yatamalizwa hapa kwa kufuata taratibu za soka,” alisema.

No comments