Simba watesa TBL Arusha
Na Mwandishi
Wetu, Arusha
TIMU ya soka ya Simba,
ambayo imeweka kambi mkoani Arusha, jana ilifanya ziara ya kutembelea
kiwanda cha Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), kilichopo jijini Arusha.
Akizungumza
katika ziara hiyo, Mwenyekiti wa Kamati ya Ufundi wa timu hiyo, Ibrahimu Masoud ‘Maestro’, alisema kuwa, wao wameamua
kufanya ziara katika kiwanda hicho, ili kujionea mambo mbalimbali yanayofanywa
na kampuni hiyo inayozalisha bia ya Kilimanjaro Premium Lager, ambayo ndio
wadhamini wakuu wa timu yao.
Alisema kuwa,
Kilimanjaro Premium Lager huwapa ushirikiano mkubwa katika mambo mbalimbali ya
kimichezo, yakiwemo magari ya usafiri, jezi na vifaa mbalimbali vya michezo,
hivyo wamefurahishwa mapokezi mazuri kiwandani hapo, na kuwaomba waendelee na
moyo huo huo wa kuthamini timu yao.
Naye, Meneja wa
bia ya Kilimanjaro, George Kavishe, kwa niaba ya TBL alisema kuwa,
wamefurahishwa sana na ujio wa timu hiyo, kwa kuamua kuacha kazi zao na kutembelea
kiwanda chao kuona jinsi wanavyofanya kazi.
Alisema kuwa, TBL
inathamini mchango wa timu za Simba na Yanga, kwa soka la Tanzania, na ndio
maana imekuwa ikizidhamini timu hizo kwa muda mrefu, huku akibainisha kuwa,
wataendelea kudhamini timu hizo hadi mwisho.
Alisema kuwa,
timu hizo hufanya mambo makubwa, kwani zimekuwa zikiwapatia vijana mbalimbali
ajira, huku akiwasihi wananchi kuendelea kuziunga mkono timu hizo, kwani ndizo zenye
wachezaji wengi wanaochezea timu ya taifa.
Kavishe
alisema kuwa, kupitia udhamini wa timu hizo, pia wamekuwa wakijitangaza sehemu
mbalimbali, ikiwemo nje ya nchi, hivyo wanasaidia kuifanya kampuni na bia ya
Kilimanjaro kuwa juu zaidi.
Wachezaji
na viongozi wa klabu ya Simba wakitembelea kiwanda cha TBL kilichopo
Arusha mwishoni mwa wiki ili kujionea uzalishaji wa bia ya Kilimanjaro
Premium Lager ambayo ndio mdhamini wao mkuu
Kocha
Mkuu wa Simba, Profesa Milovan Cirkovic akiongea na Meneja wa Bia ya
Kilimanjaro Premium Lager, George Kavishe kwenye hafla iliyofanyika
baada ya wachezaji na viongozi wa klabu ya Simba kutembelea kiwanda cha
TBL kilichopo Arusha mwishoni mwa wiki ili kujionea uzalishaji wa bia ya
Kilimanjaro Premium Lager ambayo ndio mdhamini wao mkuu.
Mratibu
wa Usalama na Afya wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) Kassena Heavy,
akiwaeleza jambo wachezaji na viongozi wa klabu ya Simba waliotembelea
kiwanda cha TBL kilichopo Arusha mwishoni mwa wiki ili kujionea
uzalishaji wa bia ya Kilimanjaro Premium Lager ambayo ndio mdhamini wao
mkuu.
Wechezaji
wa klabu ya Simba wakiwa katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa
kiwanda cha Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) kilichopo Arusha mwishoni mwa
wiki ili kujionea uzalishaji wa bia ya Kilimanjaro Premium Lager ambayo
ndio mdhamini wao mkuu
Mratibu
wa Usalama na Afya wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) Kassena Heavy,
akiwaeleza jambo wachezaji na viongozi wa klabu ya Simba waliotembelea
kiwanda cha TBL kilichopo Arusha mwishoni mwa wiki ili kujionea
uzalishaji wa bia ya Kilimanjaro Premium Lager ambayo ndio mdhamini wao
mkuu
Kocha
Mkuu wa Simba, Profesa Milovan Cirkovic akitoa neon la shukrani baada
ya wachezaji na viongozi wa klabu ya Simba kutembelea kiwanda cha TBL
kilichopo Arusha mwishoni mwa wiki ili kujionea uzalishaji wa bia ya
Kilimanjaro Premium Lager ambayo ndio mdhamini wao mkuu. Kulia kwake ni
Meneja wa Bia ya Kilimanjaro Premium Lager, George Kavishe na Meneja wa
Vifaa wa Klabu ya Simba, Kessy Hassan. Picha: Executive Solutions
No comments