Miss East Africa kuoneshwa ‘live’ na MNET
Mwakilishi wa Seychelles katika mashindano ya Miss East Africa- Annabelle Marvel Pointe (19)
Na Mwandishi Wetu
MASHINDANO ya urembo ya Afrika Mashariki yamepangwa
kuoneshwa moja kwa moja kupitia Mnet, ambapo yatashuhudiwa na watu wanaokadiliwa kufikia milion 200, kupitia televison na kwa njia ya
internet duniani kote.
Awali, mashindano hayo yanayozishirkisha nchi za
Kenya, Uganda, Ethiopia, Sudan Kusini, Tanzania, Kenya, Rwanda, Burundi,
Comoro, Shelisheli na nyingine, yalipangwa kufanyika Septemba mwaka huu, lakini
yamesogezwa mbele hadi Desemba 7.
Akizungumza jijini Dar es Salaam jana, Mkurugenzi wa
Kampuni ya Rena Events Ltd ya jijini Dar es Salaam, Rena Callist ambao ndio
waandaaji wa mashindano hayo, alisema kuwa, mashindano hayo yatafanyika katika
ukumbi wa Mlimani City jijini Dare s Salaam.
Alisema uamuzi wa kusogeza mbele tarehe ya
mashindamo hayo, ni kutoa nafasi kwa nchi ambazo hazijapata wawakilishi wao
katika mashindano hayo.
Mashindano ya Miss East Africa mwaka huu
yanatarajiwa kuwa na mvuto wa aina yake, ambapo yatashirikisha warembo kutoka
katika nchi 16 za ukanda wa Afrika Mashariki.
Nchi zilizothibitisha kushiriki mashindano hayo ni Tanzania, Kenya, Uganda, Rwanda na Burundi, wakati zilizoalikwa ni Ethiopia, Eritrea, Somalia, Djibouti, Sudan Kusini, Malawi, visiwa vya Shelisheli, Madagascar, Reunion, Comoros na Mauritius.
Alisema mashindano ya Miss East Africa yanalenga
kukuza ushirikiano na kutangaza utamaduni wa Afrika Mashariki, utalii wa
Tanzania kama nchi mwenyeji wa mashindano hayo makubwa katika ukanda huu wa
Afrika
Baadhi ya nchi zitakazoshiriki mashindano hayo ambazo
zimewatangaza wawakilishi wao ni Eritrea, Ethiopia, Uganda, Sudan Kusini,
Malawi na Shelisheli.
Callist alisema nchi zinatarajia kutangaza
wawakilishi wao kabla ya tarehe ya mwisho ambayo ni Septemba 28, mwaka huu.

Miss East Africa Uganda-Ayisha Nagudi (23)

Miss East Africa Ethiopia-Lula Teklehaimanot (19

Miss East Africa Eritrea-Rahwa Afeworki (22)
No comments