Utukufu wa Mungu yatesa nchi nzima
![]() |
Solomon Mukubwa |
ALBAMU mpya ya mwimbaji nyota wa muziki wa injili Afrika Mashariki, Solomon Mukubwa ya Utukufu wa Mungu, imesambazwa katika maduka mbalimbali nchini.
Akizungumza jijini Dar es Salaam juzi, Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotions, yenye majukumu ya kusambaza albamu hiyo, Alex Msama, alisema hivi sasa albamu hiyo inapatikana katika maduka ya Msama Music Center lililopo Kariakoo Mtaa wa Masasi na Msimbazi karibu na Kanisa la Lutherani na dula lililopo Posta katika Mtaa wa Mkwepu.
Msama alisema video ya albamu hiyo yenye nyimbo nane, audio yake ilisambazwa mapema Machi mwaka huu ni ya tatu, lakini iko tofauti na albamu zilizopita.
Mkurugenzi huyo alizitaja nyimbo zilizomo kwenye albamu hiyo ni inayopatikana katika DVD na VCD, ni Moyo tukuza Bwana, Usikate tama, Mungu nitetee, Kwa utukufu wa Mungu, Mimi ni wa Yesu, Mke sio nguo, Chunga ahadi yako, Yesu jina zuri.
"Wito wangu kwa mashabiki wa muziki wa injili ni kumuunga mkono mwimbaji huyo, kwa kununua kazi halali, waachane na kazi zilizochakachuliwa," alisema Msama.
No comments