Header Ads

ad

Breaking News

Basupa acheza filamu kupinga unyanyasaji Albino

 BAADA ya kuguswa na ukatili juu ya watu wenye ulemavu wa ngozi, msanii wa filamu nchini Omary Idd 'Basupa', hivi karibuni ataachia kazi yake mpya ya Fight for Albino.

Hatua ya msanii huyo kufanya kazi hiyo inatokana na kuguswa na matukio ya ukatili wa watu wenye ulemavu huo na kuamua kutoa filamu itakayoonesha jinsi jamii hiyo inavyopata tabu katika maisha yao ya kila siku.

Akizungumza na Dira ya Mtanzania juzi, msanii huyo alisema filamu hiyo ipo katika hatua za mwisho, ambapo mapema Juni itasambazwa maduni.

"Nimeguswa na maisha ya taabu wanayoishi wenzetu albino, baada ya kuwepo kwa watu katili wanaohatarisha maisha yao kwa kuwaua," alisema.

Hivi karibuni yamekuwepo matukio ya kikatili ya kuwakata baadhi ya viungo vya mwili wa watu wenye ulemavu wa ngozi kwa imani potofu ya biashara zao.

Hata hivyo, msanii huyo alisema filamu hiyo itaonesha madhara yanayopatikana baada ya albino kufanyiwa ukatili huo ambao anaukemia ili wanaofanya hivyo, waache kabisa.

Basupa awali alisema kazi hiyo amewashirikisha wasanii wanaochipukia katika tasnia hiyo na Albino.

No comments