Simba, Moro United kukipiga usiku
Kaseja |
Mechi
ya Ligi ya Vodacom kati ya Simba na Moro United iliyokuwa ichezwe Mei 5 mwaka huu kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam imerudishwa
nyuma hadi Jumatatu ya Aprili 23 mwaka huu kwenye uwanja huo huo na
itaanza saa 1 kamili usiku.
Mabadiliko
hayo yamefanyika ili kuipa Simba fursa ya kujiandaa vizuri kwa mechi
yao ya Kombe la Shirikisho la Afrika dhidi ya Al Ahly Shandy ya Sudan
itakayochezwa Aprili 29 mwaka huu Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kuanzia
saa 10 kamili jioni.
Pia
mechi kati ya Azam na Mtibwa Sugar iliyokuwa ichezwe Aprili 21 mwaka
huu kwenye Uwanja wa Chamazi, Dar es Salaam imesogezwa mbele hadi Aprili
22 mwaka huu kupisha mechi ya U20 kati ya Tanzania na Sudan
itakayochezwa Aprili 21 mwaka huu Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Mechi
nyingine mbili zimefanyiwa marekebisho; Coastal Union na Kagera Sugar
zilizokuwa zicheze jijini Tanga, Aprili 29 mwaka huu, mechi yao
imesogezwa hadi Aprili 30 mwaka huu ili kupisha shughuli za Mei Mosi
kwenye Uwanja wa Mkwakwani. Nazo Azam na Toto Africans zilizokuwa
zicheze Aprili 26 mwaka huu Uwanja wa Chamazi, sasa zitacheza Aprili 28
mwaka huu.
No comments