Kuzishuhudia Ngorongoro Heroes, Sudan sh. 3,000
![]() |
Sudan |
Kiingilio
cha chini cha mechi ya kuwania kucheza Fainali za Afrika kwa vijana
chini ya miaka 20 kati ya Tanzania (Ngorongoro Heroes) na Sudan
itakayochezwa Jumamosi (Aprili 21 mwaka huu) Uwanja wa Taifa, Dar es
Salaam ni sh. 3,000.
Mechi
hiyo itaanza saa 10 kamili jioni, na viingilio vingine vitakuwa sh.
5,000 kwa viti vya rangi ya chungwa, sh. 10,000 kwa VIP C na B wakati
VIP itakuwa ni sh. 15,000.
Sudan
inatarajia kuwasili leo mchana kwa ndege ya Ethiopian Airlines ikiwa na
msafara wa watu 30 na itafikia hoteli ya Rungwe iliyoko maeneo ya
Kariakoo jijini Dar es Salaam. Jioni itafanya mazoezi Uwanja wa
Kumbukumbu ya Karume.
Ngorongoro
Heroes tayari iko kambini chini ya Kocha Kim Poulsen, na leo inaendelea
na mazoezi kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. Sudan yenyewe
itafanya mazoezi kwenye uwanja huo kesho.
Kesho
(Aprili 20 mwaka huu) saa 4 asubuhi kwenye ofisi za Shirikisho la Mpira
wa Miguu Tanzania (TFF) kutakuwa na mkutano kati ya makocha wa timu
zote mbili na Waandishi wa Habari.
No comments