Mashabiki washuhudia Barcelona akilambishwa bao 1-0 na Chelsea katika nyumba ya Heinken Champions Planet iliyopo Masaki.
Na Mwandishi wetu
Ulikuwa usiku wa huzuni kwa mashabiki wa Barcelona ambao wamezoea kuiona timu yao ikiibuka na ushindi katika kila mechi inayocheza. Katika mchezo wa juzi, mashanbiki lukuki walitabiri kuwa timu hiyo ingeshinda akwa mabao mengi dhidi ya Chelsea, hata hivyo, kibao kiligeuka na matokeo kuwa kinyume pamoja na ukweli kuwa wachezaji wa Chelsea walipata tabu sana kuupata mpira kutokana na mechi hiyo kutawaliwa na Barcelona kwa asilimia 70-30.
Hata hivyo mfalme wa soka duniani, Pele alisema kuwa soka ni mabao na ndivyo ilivyokuwa kwa Chelsea wao kuachana na mambo ya kulemba na kupiga bao moja lililofungwa na nyota kutoka bara la Afrika, Didier Drogba.
George Meneja Mkuu wa Dragon Pub Sam Hurford wakiwa na meneja mkuu wa Heineken wa Tanzania Rodney Hensen dani ya nyumba ya Heineken Champions Planet Masaki
Watangazaji wa redio clouds, Millard Ayo na Reuben Ndege nao walishuhudia kipigo cha FC Barcelona ndani ya nyumba ya Heinken Champions Planet Masaki
Mmoja wa washindi walioweza kujibu maswali vizuri pamoja na kutabiri matokeo akipokea zawadi kutoka kwa akina dada wa nyumba ya Heinken Champion Planet Masaki
Mtangazaji wa MTV na Choice FM, Vanessa Mdee naye alishuhudia Barcelona akitandikwa na Chelsea katika nyumba ya Heineken Champions Planet, Masaki
Michael Mbungu akiwa amafuatilia matokeo ya mechi hiyo ndani ya chumba cha wana-habari katika nyumba ya Heineken Champions Planet, Masaki.
Baada ya kutabiri nani mshindi, jamaa alishinda boksi moja la bia ya Heineken katika nyumba hiyo.
No comments