Mwamuzi Sanya apeleka kesi mahakamani
BAADA ya Mwamuzi Martini Sanya wa Morogoro kupokea kipigo kutoka kwa mashabiki wa soka katika mechi ya Ligi Kuu Bara iliyowakutanisha Azam FC na Polisi Tanzania, mwamuzi huo amefungua kesi mahakamani.
Kwa mujibu wa Katibu Mkuu wa Chama cha Waamuzi Tanzania (FRAT), Leslie Liunda, alisema hatua ya Sanya kufungua kesi hiyo mahakamni, inatokana na kitendo hicho kufanyika baada ya kumalizika kwa mtanange huo.
Liunda alisema mwamuzi huyo alikuwa katika chumba cha kubadilishia nguo na hivyo kuzingirwa na watu ambao walimshushia kipigo.
Awali, katibu huyo alisema kitendo cha kupigwa kwa mwamuzi huyo ni kibaya na kinarudisha nyuma maendeleo ya soka nchini.
Hata hivyo, Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), limesikitishwa na kitendo hicho na kuamua kuchukua hatua kali mara watakapowabaini wahusika waliompiga Sanya .
Msemaji wa TFF, Boniface Wambura, alisema kuwa, wanaamini watawapata watuhumiwa hao, kwani anawakumbuka baadhi yao.
Alisema kama kuna wachezaji ambao walihusika katika tukio hilo, Kamati ya Nidhmau itawashughulikia kwa kufuata taratibu zilizopo.

No comments