Header Ads

ad

Breaking News

Bayern Munich yaizima Madrid usiku wa kuamkia leo

Mari Gomez, muuaji bao la pili

MUNICH, Ujerumani
BAO la dakika za mwisho lililofungwa na Mario Gomez, liliisaidia timu yake kuibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Real Madrid katika mechi ya nusu fainali ya Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya.

Franck Ribery, aliipatia timu yake bao la kwanza shuti kali akiunganisha mpira wa kona.
Lakini, Mesut Ozil juhudi zake zilifanikiwa kusawazisha bao baada ya Cristian Ronaldo kuuwahi mpira na kumpasia mfungaji wa bao hilo.

Gomez alipoteza matumaini ya sare baada ya kuifungia timu yake ya Bayern Munich bao la pili lililoiweka katika nafasi nzuri ya kutinga fainali ya michuano hiyo kwa mwaka huu.

Kocha wa Real Madrid, Jose Mourinho anajaribu kuwa kocha wa kwanza kutwaa ubingwa wa Ulaya, Europa na Ligi ya Mabingwa Ulaya mara tatu akiwa na timu tatu tofauti.

Real walionekana kama kuriridhika na sare baada ya kutumia muda mwingi kumiliki mpira eneo lao, kwa Gomez ilidhihirisha ubora wake ambapo mara kwa mara alikuwa akichezewa vibaya na mabeki wa kati wa Real Madrid Pepe na Sergio Ramos.

Lakini, kwa Cristiano Ronaldo aliyekuwa akitengeneza nafasi nyingi kwa timu yake, Gomez alionesha ubora wake kwa kufunga bao na kufikisha mabao 40 msimu huu.

Akikabiliwa na ugumu, Kocha wa Madrid, Jose Mourinho amepanga mchezo wa marudiano kuwa mgumu, kwani Real, inayoongoza kwa zaidi ya pointi nne dhidi ya Barcelona kwenye La Liga, watasaifiri mpaka Nou Camp Jumamosi, wakati Bayern itawapumzisha wachezaji wake kwani tayari wamepoteza matumaini ya kutwaa ubingwa wa Bundesliga.

Lakini, upande wa Kocha Jupp Heynckes, ambapo ushindi wao ni wa thamani kwao na wanaangalia kuwa timu ya kwanza kucheza kwenye uwanja wake mechi ya fainali.

Kabla ya Bayern kupata bao la kuongoza, kipa wake Manuel Neuer, alifanikiwa kuokoa mpira uliopigwa na Karim Benzema na Ribery alianguka wakati wakiwania mpira na Ramos ndani ya eneo la penalti.
Mpira wa kona uliopigwa na Toni Kroos uligonga kifuani kwa Ramos na Ribery alikuwa wa kwanza kulalamika, alipiga shuti lililowapita mabeki wa Madrid na kipa Iker Casillas.

Ramos na Pepe, walikosa raha kwa kishindo cha Gomez, ambapo mshambuliaji huyo wa Bayern alipiga shuti lililompita kipa Casillas na kuwa bao la pili. Cristiano Ronaldo alishindwa kufunga bao mara nne katika mechi 17.
Kocha Bayern Munich, Jupp Heynckes: "Wachezaji wangu walionesha kile nilichowafundisha, tamaa na njaa kwa mafanikio.

"Nadhani zaidi tulistahili kushinda, kwasababu tulicheza kwa mpangilio na kwa akili zaidi."
Kocha wa Real Madrid, Jose Mourinho: "Bao la pili lilikuja toafuti na mipango yetu. Tulicheza vizuri kipindi cha kwanza na kipindi cha pili, mchezo ulikuwa sawa na sikupenda iwe hivyo.

"Ulitawaliwa na timu zote mbili, na hakuna aliyekuwa akiamini atashinda 2-1, lakini hiyo ndiyo soka na tutacheza mechi ya marudiano nyumbani.

Bayern Munich: Manuel Neuer, Holger Badstuber, Jerome Boateng, David Alaba, Philipp Lahm, Bastian Schweinsteiger/Thomas Müller, Luis Gustavo Dias, Mario Gomez, Toni Kroos, Franck Ribery, Arjen Robben

Real Madrid: Iker Casillas, Sergio Ramos, Pepe, Fabio Coentrao, Alvaro Arbeloa, Sami Khedira, Xabi Alonso, Karim Benzema/Gonzalo Higuain, Mesut Ozil/Marcelo, Cristiano Ronaldo, Angel Di Maria/Esteban Granero.

No comments