Azam FC waitaka ubaya Simba
![]() |
Azam FC |
UONGOZI wa klabu ya Azam FC ya jijini Dar es Salaam, umetamba kuibuka na ushindi katika mechi zake nne za Ligi Kuu Bara zilizobaki.
Timu hiyo inayoshika nafasi ya pili katika msimamo wa ligi hiyo, wao wanawaombea mabaya vinara wa ligi hiyo Simba, wachapwe ama kutoka sare katika moja ya michezo yake iliyobaki.
Msemaji wa Azam FC, Jaffari Iddi, alisema kuwa, wakifanikiwa kuibuka na ushindi katika mechi zilizosalia, itawasaidia kupata moja ya nafasi za kuwakilisha nchi kwenye michuano ya kimataifa.
Iddi alisema kwa upande wao, wanaiombea timu ya Simba ifungwe mechi mbili ili waweze kutwaa ubingwa wa Bara msimu huu. Azam FC mpaka sasa imejikusanyia pointi 50, huku ikibakiwa na mechi tatu ambazo zitaiwezesha kufikisha pointi 59.
Wakati huo huo, timu za Simba, Azam na Yanga zikiwa juu katika msimamo wa ligi hiyo, timu za Villa Squad, African Lyon na Moro United zipo katika hatari ya kushuka daraja, baada ya kuwa mkiani mwa msimamo huo.
No comments