25 TWIGA STARS KAMBINI APRILI 20
![]() |
Twiga Stars wakiwa na Rais Jakaya Kikwete |
Kocha
Mkuu wa Twiga Stars, Charles Boniface Mkwasa ameita wachezaji 25
watakaoingia kambini kesho (Aprili 20 mwaka huu) kwa ajili ya mechi ya
kirafiki dhidi ya Zimbabwe inayotarajiwa kuchezwa Aprili 28 mwaka huu
jijini Dar es Salaam.
Mechi
hiyo ni sehemu ya maandalizi ya Twiga Stars kabla ya mechi ya
mashindano ya Afrika kwa Wanawake (AWC) dhidi ya Ethiopia itakayochezwa
Mei 26 mwaka huu jijini Addis Ababa kabla ya timu hizo kurudiana jijini
Dar es Salaam wiki mbili baadaye.
Baada
ya kuripoti kambini jioni, wachezaji hao watafanyiwa vipimo vya afya
(medical examination) siku inayofuata (Aprili 21 mwaka huu) na kuanza
mazoezi Aprili 22 mwaka huu. Kambi ya timu hizo itakuwa kwenye hosteli
za Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) ya Ruvu mkoani Pwani.
Wachezaji
walioitwa ni Amina Ally kutoka Sekondari ya Lord Baden, Asha Rashid,
Aziza Mwadini (New Generation, Zanzibar), Etoe Mlenzi (JKT Mbweni),
Evelyne Sekikuto (Mburahati Queens), Fadhila Hamad (Uzuri Queens),
Fatuma Bashiri (Simba Queens), Fatuma Khatib (Mburahati Queens) na
Fatuma Mustafa (Sayari).
Wengine
ni Fatuma Omari (Sayari), Hanifa Idd (Uzuri Queens), Maimuna Said (JKT
Mbweni), Mariam Aziz (Tanzanite), Mwajuma Abdallah (Tanzanite),
Mwanahamisi Omari (Mburahati Queens), Mwanaidi Tamba (Mburahati Queens),
Mwapewa Mtumwa (Sayari) na Rehema Abdul (Lord Baden).
Kikosi
hicho pia kina akina Rukia Khamis (Sayari), Semeni Abeid (Tanzanite),
Siajabu Hassan (Evergreen), Sophia Mwasikili (Luleburgaz Spor Kulubu,
Uturuki), Veneranda Mtamo (Tanzanite), Zena Khamis (Mburahati Queens) na
Zena Said (Uzuri Queens).
No comments