TASWIRA ZA MPAMBANO KATI YA YANGA NA KAGERA SUGAR KWENYE UWANJA WA KAITABA BUKOBA
Mkuu wa mkoa wa Kagera Kanali Fabian Masawe akikagua timu kabla ya
kufanyika kwa mpambano wa ligi kuu ya Vodacom kati ya timu ya Yanga na
Kagera Sugar kwenye uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba jana ambapo timu ya
Kagera Sugar iliikandamiza Yanga goli 1-0 na kutoka uwanjani kifua
mbele.
Picha kwa hisani ya www.bukobawadau.blogspot.com
Kocha wa timu ya yanga Bw. Kostadic Papic akiwa katika benchi la ufundi
la timu hiyo na wachezaji wake kwenye uwanja wa Kaitaba jana.
Wachezaji wa timu ya Yanga wakinywa maji wakati wa mpambano wao.
Kikosi cha timu ya Kagera Sugar kikiwa katika picha ya pamoja.
Mashabiki wa mpira wa miguu wakiwa wamefurika kwenye uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba jana.
Mmoja wa mashabiki anayesadikika ni mshabiki wa timu ya Simba akionekana kuwatania watani wake mashabiki wa timu ya Yanga
Nyomi la mashabiki likifuatilia mchezo huo.
Benchi la ufundi la timu ya Kagera Sugar.
Mdau MC Baraka
wa Bukobawadaublog kulia akiwa na wadau wengine kwenye uwanja wa
Kaitaba kushoto ni Sadik Galiatano , Enock na mmoja wa mashabiki wa
Yanga.
No comments