Header Ads

ad

Breaking News

TFF yasubiri ripoti ya Kocha Poulsen


SHIRIKISHO la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), linasubiri ripoti ya Kocha Mkuu wa timu ya Taifa (Taifa Stars), Jan Poulsen, itakayoelezea majumuisho ya matokeo ya mechi zote zilizokuwa za kuwania kufuzu kucheza mashindano ya Mataifa ya Afrika, mwakani (CAN 2012) ili kujua wapi waboreshe.

Timu hiyo jana usiku, ilizimwa ndoto zake kushiriki kwa mara nyingine michuano hiyo tangu ipite miaka 20,  baada ya kukubali kichapo cha mabao 3-1, kutoka kwa wenyeji Morocco.

Katibu Mkuu wa shirikisho hilo, Angetile Osiah,  amesema wameyapokea matokeo hayo kama changamoto, ambapo  wanatakiwa kujua wapi walipojikwaa ili mashindano yajayo wafanye vizuri.

Amesema licha ya kwamba, nchi haikufuzu ni lazima atawasilisha ripoti yake, ambapo sababu inaweza ikawa maandalizi hayakuwa yakutosha, hivyo wanasubiri ripoti na mambo mengine yatafuata.

Amesema baada ya kuondolewa katika mashindano hayo, nguvu zao wanazielekeza katika kuwania kucheza fainali za Kombe la Dunia, ambapo Novemba 11, wataanza kwa kucheza na Chad ugenini.

No comments