Header Ads

ad

Breaking News

Swahili Fashion Week yapeleka wawili Angola



Foto: Manju Msita


JUKWAA la maonesho ya mavazi ya Swahili Fashion Week limetoa wawakilishi wawili watakaotangaza mavazi ya kiswahili katika tamasha la mavazi litakalofanyika nchini Angola Oktoba 14, mwaka huu.

Wawakilishi hao ni Gabriel Mollel na Manju Msita, ambao wote ni wabunifu wanaoshiriki katika jukwaa la maonesho ya Swahili Fashion Week.

Ofisa Habari wa Swahili Fashion Week,  Enstenium Mgimba, alisema onesho hilo ambalo litajulikana kwa jina la Fashion Business Angola, litafanyika katika mjini Filda, Luanda, ambapo wataanadamana na mwazilishi wa Swahili Fashion Week,  Mustapha Hasanali.

Amesema Hassanali aliwahi kuonesha mavazi yake mwaka jana nchini Angola, ambapo mwaka huu wamepata mwaliko mwingine wa kushiriki maonesho hayo.

Ofisa huyo amesema maonesho hayo yatasaidia Jukwaa la Swahili kutambulika katika nchi zinazoongea lugha ya kireno.

 Amesema Swahili Fashion Week ina programu mbadala na Msumbiji Fashion week, Festival of Arts an Fashion (FAFA) ya Kenya na Angola, yatawawezesha wabunifu kuonesha kazi zao na kwamba wabunifu kama Jamila Swai, Robbi Maro na Msita Manju, wamewahi kuonesha kazi zao katika matamasha hayo.

Amesema katika maonesho hayo, Hassanali atashiriki kama washiriki wengine watakaoonesha mavazi yao na kwamba,  wabunifu hao wanatarajia kuondoka nchini kesho.

Enstenium amesema jukwaa la Swahili Fashion Week, mara baada ya kuzinduliwa jijini Arusha Oktoba 8, mwaka huu,  maonesho hayo yatafanyika tena jijini Dar es Salaam Novemba 10 hadi Novemba 12,  mwaka huu.

Wadhamini wa maonesho hayo ni Southern Sun, Precision Air, Baraza la Sanaa Taifa (BASATA), Amarula, Ultimate Security, Redd's, Image Master na Global Outdoor.

No comments