Header Ads

ad

Breaking News

Naibu Waziri ataka wanafunzi wazingatie michezo

                                        Naibu Waziri, Kassim Majaliwa

WANAFUNZI nchini wametakiwa kuongeza juhudi  katika michezo ili kujiweka katika nafasi nzuri ya kunufaika na sekta ya michezo katika ajira.

Wito huo ulitolewa juzi na  Naibu Waziri  wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu-TAMISEMI,  Kassim Majaliwa, wakati alipokuwa akizindua mradi wa michezo kwa wote unaoendeshwa na Taasisi ya Michezo ya Amer kwa ufadhili wa nchi ya Finland.

Finland imekuwa ikitoa  vifaa mbalimbali vya michezo kwa shule za msingi na sekondari  mkoani Lindi.

Majaliwa amesema wakati umefika  kwa wanafunzi  kupenda michezo  kwani licha ya kupata afya bora,  pia ni ajira na kujenga mahusiano.

Majaliwa amewataka wazazi na walezi kuiunga mkono taasisi ya Amer ili iweze kufanikiwa katika  malengo yao ya kuinua vipaji vya michezo kwa vijana.

Amewataka walimu wa michezo kutoa ushirikiano kwa   wanafunzi wanaopenda michezo , kwa kuwafundisha kanuni na sheria.

Amesema iwapo walimu na wanafunzi watajizatiti kwenye michezo, wataweza kusaidia kupunguza utoro shuleni na kuongeza mahudhurio madarasani.

No comments