Header Ads

ad

Breaking News

Oljoro yaipumulia Simba, yaishusha Azam

TIMU ya soka ya Oljoro JKT, leo iliichapa Coastal Union bao 1-0, katika mechi ya Ligi Kuu Bara iliyochezwa kwenye Uwanja wa Sheikh Amri Abeid mjini Arusha na kupanda mpaka nafasi ya pili katika msimamo wa Ligi Kuu Bara.

Kwa ushindi huo, Oljoro imepanda mpaka nafasi ya pili ikiiacha Azam FC ikishuka mpaka nafasi ya nne, nyuma ya Mtibwa Sugar,ambao waliibuka na ushindi wa mabao 2-1, dhidi ya Ruvu Shooting kwenye Uwanja wa Manungu Turiani, Morogoro, wakiwazidi kwa uwiano wa mabao.

Mabao ya Mtibwa Sugar yalifungwa na Thomas Morris dakika ya 73 na Mohamed Mkopi dakika ya 80, wakati Ruvu lilifungwa na Raphael Kyala dakika 17.

Kutoka Dar es Salaam kwenye Uwanja wa Azam Chamazi, Villa Squad na Moro United zilitoka sare ya bao 1-1. Villa ilipata bao lake kwa mkwaju wa penalti dakika ya 17, uliopigwa na Nsa Job, baada ya kuchezewa vibaya na kipa Jackson Chove. Lakini, Moro walisawazisha dakika ya 90, kupitia kwa Omega Seme.

Kutoka Dodoma, Polisi Dodoma na Toto African zilitoka suluhu kwenye Uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma.

No comments