Mabingwa mpira kikapu nchi za A/Mashari na Kati kuwasili Ijumaa
Timu zilizonyakua ubingwa katika mchezo wa kikapu katika nchi za Afrika Mashariki na kati, zinatarajiwa kuanza kuwasili kuanzia Oktoba 7 mpaka 8, mwaka huu kwa ajili ya mashindano ya Klabu Bingwa kwa nchi hizo yatakayofanyika nchini.
Mashindano hayo yanatarajia kuanza kutimua vumbi Oktoba 9 hadi 16, mwaka huu katika Uwanja wa ndani wa Taifa na Uwanja wa Don Bosco Upanga, Dar es Salaam ambavyo vimeteuliwa kwa ajili ya mtanange huo.
Katibu Mkuu wa Shirikisho la Mpira wa Kikapu Tanzania (TBF), ambaye pia ni Mjumbe wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT), Alexander Msofe amesema maandalizi ya mashindano hayo yanaendelea vizuri.
Amesema timu kutoka nchi za Uganda na Kenya, zimethibitisha kutua nchini Oktoba 7 huku Ethipia na timu nyingine zinatarajiwa kutua Oktoba 8, mwaka huu.
Msimu uliopita mashindano hayo yalifanyika Burundi ambapo timu ya Kenya Port Authority (KPA), ilitwaa ubingwa.

No comments