Mbunge wa Morogoro Mjini awaasa waandishi
MBUNGE wa Jimbo la Morogoro Mjini, Abood Aziz, amewataka waandishi wa Habari za Michezo nchini kuandika habari za michezo mbalimbali, badala ya kuzingatia zaidi mpira wa miguu.
Akifungua mafunzo ya siku mbili kwa waandishi wa habari za michezo yaliyoandaliwa na Chama cha Waandishi wa Habari za Michezo Tanzania (TASWA), Abood alisema kama waandishi watageukia michezo mingine, wananchi watapata nafasi ya kujui michezo mingine.
Katika semina hiyo iliyowashirikisha waandishi 40, kutoka mikoa ya Morogoro, Pwani na Dar es Salaam, Mbunge huyo alisema wananchi wanapaswa kujua sheria na kanuni ya michezo mingine, hivyo ni kazi ya waandishi kuwaelimisha.
Alisema vyombo vingi vya habari vimekuwa vitoa nafasi kubwa kwa baadhi ya michezo, hali ambayo inadidimiza michezo mingine.
"Nawashauri waandishi muache ushabiki, mfano Kocha wa timu ya taifa anapomwacha mchezaji wa klabu fulani, nyie mnampinga, haileti picha nzuri," alisema.
Mafunzo hayo yatafungwa leo na Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Joel Bendera, yaliandaliwa na TASWA kwa lengo la kuwakumbusha waandishi majukumu yao, yalianza jana na kumalizika leo katika ukumbi wa Morogoro Hoteli.

No comments